Yanga SC yaanza na Ushindi wa kwanza kwenye Mashindano ya Kimataifa Msimu huu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, February 10, 2018

Yanga SC yaanza na Ushindi wa kwanza kwenye Mashindano ya Kimataifa Msimu huu.

Golikipa wa Timu ya St Louis.

Mashabi walioingia uwanja wa taifa –walishuhudia dk 90 zikimalizika kwa Mchezaji wa klabu ya Yanga, Juma Mahadhi akiisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa bao 1 – 0 dhidi ya St Louis kwenye mchezo huo wa Ligi ya vilabu Bingwa Afrika.

Mchezaji Juma Mahadhi amefanikiwa kuipatia bao timu hiyo wakati wa kipindi chapili baada ya kuchukua nafasi ya Ibrahim Ajib aliyekwenda benchi.
Kwa matokeo hayo sasa timu hizo mbili zinatarajiwa kukutana tena mchezo wa marudiano baada ya wiki moja huko Shelisheli.

Hapo kesho Jumapili,February 11, 2018, Simba SC watacheza mechi ya kimataifa dhidi ya Gendermerie kutoka Djibouti katika mechi ya kwanza Kombe la Shirikisho ambao utapigwa kwenye Uwanja wa Taifa.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad