Jesica
akiugulia uchungu katika korido ya hospitali.
|
…Akisaidiwa na manesi.
|
Mtoto
akiwa amezaliwa salama-salimini.
|
…Akiwa
amelala chini, amejifungua.
|
Travis
akifurahia kichanga chake.
|
Jesica
na Travis wakipongezana.
|
Mtoto, Max, akiwa na afya njema.
|
Jesica
na Travis wakiwa na binti zao sita wanaofurahia kumpata kaka yao.
JESICA
HOGAN, mama wa watoto sita mkazi wa Riley, Kansas, Marekani, amejifungua mtoto
pekee wa kiume katika korido ya hospitali ambayo alikuwa anawahishwa kwenda
kujifungua.
Mtoto huyo
aliyeleta furaha katika familia hiyo ambayo ilikuwa na mabinti mtupu, anaitwa
Max, ambaye alizaliwa akiwa salama na mwenye afya njema.
Mwanamke
huyo aliyejifungulia katika Hospitali ya Via Christi, ya Manhattan, Kansas,
alisema alikuwa hana uhakika wa tarehe ya kujifungua, hivyo hakujua ni lini
uchungu ungelianza. Alikuwa nyumbani wakati chupa ilipovunjika kunako saa
tisa usiku ambapo mumewe, Travis, alimkimbiza hospitali.
Mara tu
baada ya kuingia katika korido ya hospitali hiyo, Jesica alihisi mtoto alikuwa
ameanza kutoka, hivyo akaanza kuvua suruali yake wakati kichwa cha mtoto
kilianza kujitokeza. Walianza kusaidia na mumewe hapohapo kwenye korido
ambapo alilala chini kabla ya manesi kuja na kumsaidia.
“Nilikuwa
sifahamu hasa siku halisi ya kujifungua, lakini siku hiyo nilijua imefika,
nikamwambia Travis naye akaamua kunikimbiza hospitali.” anasema Jesica ambaye
anasema alisahau hata kuvaa viatu kwa ajili ya uharaka.
|
No comments:
Post a Comment