Jeshi la
Polisi Mkoani Arusha limepata miili ya watu 11 waliofariki kwenye ajali ya
ndege ndogo ya Coastal Aviation iliyotokea jana November 15,
2017 katika eneo la Embakaai Wilayani Ngorongoro wakati ikiwa safarini
kuelekea Serengeti.
Ndege hiyo
ilipaa kutoka uwanja mdogo wa Arusha saa nne na dakika 10 asubuhi kuelekea
uwanja wa Ndege Kilimanjaro (KIA) na Shirika la Ndege la Coastal
(Coastal Aviation) katika taarifa yake kuhusu ajali hiyo limesema kuwa watu wote 11 waliokuwa
katika ndege hiyo wamefariki dunia.
Coastal wameeleza
kuwa, ndege yao, Cessna Caravan ilipata ajali majira ya saa 5 asubuhi kwa saa
za Afrika Mashariki na Kwa sasa unafanyika uchunguzi katika eneo la tukio na
kuwa, taarifa zaidi kuhusu chanzo cha ajali hiyo watazitoa mara taarifa kamili
zitakapopatikana.
No comments:
Post a Comment