![]() |
…Akiwa
na Sifael Paul na Mhariri Mwandamizi wa gazeti la Uwazi, Elvan Stambuli
(kushoto) wakati wa mahojiano kuhusu yaliyompata.
‘Klip’ya mnada huo ilianza kuwa maarufu
mtandaoni. Kipande cha video alichosikika Dk. Louis akisema ‘milioni 900
itapendeza,’ ndicho kilikuwa gumzo zaidi.
Kila mtu akawa anaweka vituko mbalimbali kwa
kuchombeza na ‘milioni 900 itapendeza’.
Mitandao yote ya kijamii ‘ikachafuka’ na watu
wote wakayatupa mambo yote yaliyokuwa yanaendelea nchini, hii ndiyo Tanzania
yetu.
Amani linakuletea baadhi ya matukio makubwa
ambayo kama si Dk. Louis yangeweza kushika hatamu katika mitandao na vyombo vya
habari.
NDOA YA UWOYA, DOGO JANJA
Kabla ya tukio la Dk. Louis ndoa ya Mbongo
Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ na muigizaji Irene Uwoya ilikuwa gumzo.
Watu wengi walikuwa wakijadili tofauti
wengine walikuwa wakisema kwamba ni ndoa ya kweli au feki.
Uwoya alisema si ndoa ya kweli lakini Dogo
Janja alikomaa kuwa ni ndoa ya kweli. Ghafla tu, upepo ukageuka na kila mmoja
akawa anajadili ‘mia tisa itapendeza.’
NAPE NA MIRADI YA SERIKALI
Kutoka Bungeni Dodoma, Mbunge wa Mtama, Nape
Nnauye ‘alikinukisha’ kwa kuikosoa serikali kwa kutoshirikisha sekta binafsi
katika miradi mikubwa. Akaeleza kwamba kama serikali itaendelea kuikumbatia
miradi yote ya fedha nyingi, kuna hatari kubwa ya kuwepo kwa anguko la uchumi
kutokana na ongezeko la deni la taifa.
Nape ambaye ni mbunge wa Chama cha Mapinduzi
(CCM), aliicharukia vilivyo serikali inayoongozwa na chama chake hali ambayo
isingekuwa Dk. Louis, angejadiliwa sana.
MAGUFULI UGANDA
Ziara ya Rais Dk. John Pombe Magufuli nchini
Uganda ilikuwa na mambo mengi makubwa likiwemo suala zima la uzinduzi wa ujenzi
wa mradi wa bomba la mafuta ghafi la Hoima – Tanga wenye urefu wa kilometa
1,443 zikiwemo 1,115 zitakazojengwa ndani ya ardhi ya Tanzania, uliogharimu
dola za Marekani bilioni 3.55 lakini kwa Dk. Louis, ishu hiyo haikujadiliwa kwa
uzito wake.
TUKIO LA LISSU
Bungeni pia suala la kushambuliwa kwa Mbunge
wa Singida Mashariki, Tundu Lissu liliibuliwa na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.
Mbowe alilibua katika kipindi cha maswali na
majibu kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitaka kuruhusiwa kwa wachunguzi wa
kutoka nje.
Hata hivyo, Waziri Mkuu, Majaliwa alisema ni
vyema suala hilo likazungumzwa kwa ujumla wake na matukio mengine na kusisitiza
kuwa vyombo vya dola havijashindwa kuchunguza tukio hilo. Tukio hilo nalo
halikujadiliwa kwa upana wake.
NYALANDU KUANZA KAZI CHADEMA
‘Bilionea’ huyo pia amezima tukio la
aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu kuanza kazi kwa
mara ya kwanza akiwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ‘Chadema,’ mkoani
Mtwara ambako alitambulishwa na Mwenyekiti Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe.
Nyalandu alijitokeza rasmi kwenye kampeni za
udiwani za chama hicho katika Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani kata
ya Reli, Jumapili iliyopita.
NENO LANGU
Watanzania wanapaswa kujikita zaidi katika
masuala ya msingi katika kipindi husika kwani kuna uwezekano tukawa
tunashabikia vitu visivyoleta tija, tukashindwa kutatua changamoto kubwa za
taifa.
|
Thursday, November 16, 2017

‘900 Itapendeza Zaidi’ yayazima Matukio 5.
Tags
# DONDOO
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
DONDOO
Labels:
DONDOO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment