![]() |
Maafisa wa jeshi la wanamaji wamesema
kwamba haikubaliki kwamba mmoja wa marubani wake alitumia ndege moja ya kijeshi
kuchora uume wa mwanadamu angani.
Mchoro huo
uliokuwa katika kaunti ya Okanogan magharibi wa jimbo la Washington nchini
Marekani ulizua hisia nyingi katika mitandao ya kijamii.
Lakini
makomando katika kituo hicho cha wanamaji kilichopo katika kisiwa cha Whidbey
hawakuona ucheshi wake na sasa wameanzisha uchunguzi.
Msemaji wa
kambi hiyo ya kijeshi alithibitisha kuwa ndege iliohusika kuchora uume huo kwa
kutumia moshi wake ni ile ya Boeing EA-18G Growlers.
Onyo: Baadhi ya watazamani huenda wakaona picha hizi kama
zisizo na maadili.
|
![]() |
Rubani wa
ndege ya Marekani alichora Uume angani.
Ndege hiyo
hutumika maalum kwa vita vya kielektroniki na inaweza kusafiri mara mbili kasi
ya sauti.
Msemaji
Thomas Mills aliambia BBC : Mimi kama mwanamaji tunawapatia heshima kubwa
marubani wetu na hili halikubaliki hata kidogo.
Watazamaji
waliokuwa chini ardhini walichekeshwa na mchoro huo.
|
No comments:
Post a Comment