Serikali ya
Jamhuri ya Burundi imesema ipo tayari kutoa ushirikiano wa hali na mali katika
kuhakikisha zoezi la urejeshwaji wa wakimbizi waliopo nchini Tanzania wanarejea
nchini Burundi kwa haraka ili wakaijenge nchi yao.
Haya
yamezungumza na Waziri wa mambo ya Ndani na Mafunzo ya Uzalendo kutoka Jamhuri
ya Burundi Mhe. Pascal Barandagiye, alipozuru katika kambi za Nyarugusu, Nduta
na Mtendeli kutoa ujumbe wa kuwaasa kurejea wakimbizi nchini kwao Burundi.
Tangu zoezi
la urejeaji wa wakimbizi lilipoanza mwezi septemba 2017 kwa awamu ya kwanza
jumla ya wakimbizi 8347 wameshasaidiwa kurejea nchini kwao Burundi sawa na
asilimia 100.3 ya lengo ya urejeshwaji kwa awamu ya kwanza.
Aidha,
mwanzoni mwa mwezi Novemba wakimbizi wapatao 33,948 walijiandikisha kurejea
nchini kwao Burundi lakini kutokana na kasi ndogo na taratibu ndefu
zinazofanywa na Shirika la kuhudumia wakimbizi Duniani UNHCR wakimbizi
waliojiandikisha wameanza kusitisha nia yao ya kurejea kwani hawaoni jitihada
zinazofanywa kuwarudisha, ambapo jumla ya wakimbizi 735 kati ya 33948
wamesitisha nia yao ya kureja kwa hiari.
Hali hii
inatajwa na viongozi wa Burundi kuwa inachelewesha zoezi kwani wakimbizi
wanaorejeshwa kwa mujibu wa mpango wa urejeaji ni ndogo. Mhe. Pascal
Barandagiye amesema serikali ya yake ipo tayari kutoa magari kwaajili ya
kuwasafirishwa wakimbizi kurudi nchi mwao, pamoja na kuwapa huduma muhimu za
kibinadamu.
“zoezi la urejeshaji wa Wakimbizi kwa hiari
linaenda polepole mno tofauti na matarajio, shirika la kuhudumia wakimbizi duniani
UNHCR linaenda kwa kasi ndogo tofauti na ilivyotarajiwa, hivyo kutokana na
zoezi hilonkuenda taratibu Serikali ya Burundi ipo tayari kutoa magari, fedha
na huduma nyingine za kibinadamu ili kusaidia kuweza kuharakisha zoezi la
kurejesha wakimbizi waliojiandikisha kurejea kwa hiari nchini Burundi”
alisisitiza Barandagiye.
Akiongea
katika nyakati tofauti tofuti katika kambi za nyarugusu, nduta na mtendeli,
amewahakikishia wananchi wa kuwa Amani
nchini mwao ipo ya kutosha hakuna vurugu na serikali ya Burundi inawahitaji ili
warejee kuenga taifa lao hakuna haja ya kuendelea kubaki makambini.
Wakimbizi
wakiongea kwa nyakati tofauti wamemhakikishia kuwa bado wanapenda nchi yao
Burundi, na wanatamani kurejea Burundi, lakini changamoto inayowakabili hadi
kukata tamaa ya kurudi ni taratibu ndefu zinazowachelewesha kurejeshwa mara tu
baada ya kujiandikisha
Akiongea kwa niaba ya Wakimbizi walioko kambi
ya Nduta Bw. Suleima Hamisi (65) ambaye amekuwa Mkimbizi mara Sita kwa nyakati
tofauti tangu mwaka 1972 alisema “ Sisi tulishajiandikisha Zaidi ya miezi mine
sasa ili tuweze kurejeshwa cha kushangaza hadi sasa badotupo makambi” ameiomba serikali ya Burundi na Tanzania na
Shirika la kuhudumia wakimbizi wakae na kuzungumza kwa pamoja juu ya
mustakabali wa kuwarejesha haraka wenye nia ya kurudi Burundi.
Akitoa
taarifa kwa Waziri wa mambo ya ndani na mafunzo ya uzalendo wa Burundi na Naibu
waziri wa mambo ya ndani wa Jamuhuri ya Muungani wa Tanzania, Mkuu wa Kambi ya
Nyarugusu ikiyopo Wilayani Kasulu alisema kumekuwa na mwitikio Mkubwa wa
wakimbizi wanao jiandikisha kurejea kwa hiari nchini Burundi lakini changamoto
imekuwa taratibu ndefu zinazochelewesha kurejea kwao zinawafanya baadhi yao
kuahirisha kurejea kutokana na kusubiri kwa muda murefu.
Serikali ya
Burundi pia imedai Shirika la kuhudumia wakimbizi Dunia UNHCR linatakiwa
kubadilisha utaratibu wa kuwapatia au kuwagawia vyakula na pesa wakimbizi
wanapokuwa wanarejea wameomba zoezi hilo lifanyike wakati tayari wakimbizi
wakishapatiwa nyumba na maeneo yao ya makazi kuepusha kukaa kwa muda mrefu
kwenye vituo vya kuwapokelea.
Naye Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema serikali ya
Tanzania itahakikisha wakimbizi waliopo nchi wanahifadhiwa kwa mujibu wa
makubaliano ya taratibu za kimataifa na wale wanaopenda kurejea kwa hiari
itashirikiana na UNHCR, nchi ya Burundi
ili kufanikisha zoezi hilo.
Hatua ya kuwarejesha wakimbizi katika nchi yao ya
asili ni moja kati ya suluhisho la kudumu la ukimbizi kwa mujibu wa sharia ya
kimataifa ya wakimbizi ya mwaka 1951 na Sheria ya Wakimbizi ya Tanzania yam
waka 1998 kifungu Na. 3
Zoezi la
kurejea kwa wakimbizi nchini mwao waliopo Tanzania lilianza kuratibiwa mara tu
baada ya tamko la viongozi rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. John
Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Burundi Pierre Nkurunzinza walipo kutana
Mwezi Julai 20, 2017 na kutamka kuwa wakimbizi waliopo Katika Makambi nchi
Tanzania warejee nchini kwao kwani Burundi kuna amani ya kutosha.
Hadi sasa
idadi ya wakimbizi walioko katika Mkoa wa Kigoma ni 210,005 na waomba hifadhi
26,410, kati ya hao 95,243 wapo kambi ya Nduta, 48147 kambi ya Mtendeli na
66615 Nyarugusu, aidha waombahifadhi wote wapo katika kambi ya nduta.
|
No comments:
Post a Comment