
![]() |
The Gunners
waliongeza bao la pili dakika tano baadaye , baada ya mshambuliaji wa Chile,
Sanchez kufunga krosi iliopigwa na Alexandre Lacazzette akiwa amekaribia goli.
Sanchez
alikuwa na fursa ya kuongeza bao la tatu lakini shambulio lake likapanguliwa na
Hugo Lloris.
Fursa nzuri
ya wageni hao ilimwangukia kiungo wa kati Christian Eriksen katika kipindi cha
kwanza lakini shambulio la kimo cha paka la raia huyo wa Denmark liligonga
chuma cha goli huku kipa Petr Cech akiruka na kuokoa kichwa kilichopigwa na
Eric Dier.
|

![]() |
Ushindi huo
sasa umeifanya Arsenal kubaki nafasi ya 6 katika Msimamo wa Ligi msimu huu 2017/2018 wakiwa na Pointi 22 juu ya kikosi cha Mauricio Pochettino chenye Pointi 23 nafasi ya 4.
|

No comments:
Post a Comment