|
WENGI
huwa wanajiuliza mwanamke au mwanaume, umri wa mwisho kushiriki tendo la ndoa
ni upi?
Ukiwa mzee unaweza kushiriki tendo hili hadi lini? Kuna madhara yoyote
kwa bibi au babu kikongwe kuendelea kushiriki?
Katika kujibu maswali haya ni
vema kupitia baadhi ya tafiti ambazo zilifanyika duniani ili kupata ukweli wa
maswali.
HALI HALISI ILIVYO
Kila
binadamu ambaye ameshazoea kuwa karibu na mwenza wake siku zote
angependa
iwe hivyo.
Hii ni pamoja na kuendelea kuwa na hamu ya tendo la ndoa, uwezo wa
kufanya tendo la ndoa na kuridhishwa na tendo la ndoa, lakini kadiri umri
unavyoongezeka yanatokea mabadiliko ambayo yanaweza kuleta matatizo
usiyotarajia.
MABADILILIKO YA KAWAIDA
UZEENI
Mabadiliko
ya kawaida uzeeni humbadilisha mwanaume na mwanamke muonekano wao katika
maumbile kuanzia nje hadi sehemu za siri.
Mabadiliko haya ya kawaida pia
hupunguza mvuto wa kuwa na hamu ya tendo la ndoa.
Mwanamke anapozeeka huhisi
mabadiliko yasiyo ya kawaida ukeni ambapo uke huanza kuwa na kina kifupi na
upana wa mwingilio hupungua, ngozi ya ukeni huwa nyembamba sana tofauti na
awali na huwa ngumu, haitanuki kama mwanzo.
Majimaji ya ukeni yanayolainisha
uke huanza kupungua taratibu. Hali hii huondoa uwezo wa kufanya tendo la ndoa
na hali ya kulifurahia.
Kwa
hiyo ukiona hali hii inaanza kukutokea basi wasiliana na daktari wako. Kwa
upande wa wanaume wanapoanza kuzeeka nguvu za kiume huanza kupungua na kupotea,
hali hii ndio kiashiria kikubwa cha kuzeeka kwa mwanaume.
Upungufu wa nguvu za
kismet ambao kitaalamu tunaita Erectile Dysfunction humfanya mwanaume uume wake
usiwe na nguvu za kutosha kuhimili ufanyaji wa tendo la ndoa kwa muda mrefu.
Unaposimama
uume hauwi imara na mkubwa kama inavyotakiwa na huwa unapwaya, ingawa tatizo
hili siyo tu hutokea uzeeni.
UMRI WA UZEE
Labda
tujiulize, umri wa uzee ni upi ambao tunasema mtu anashindwa au anaanza
kushindwa kufanya tendo la ndoa?
Kwa mujibu wa utafiti, umri wa uzee ambao tunategemea
mwanaume na mwanamke wanaweza kupata matatizo haya ni kuanzia miaka sitini
endapo watu hawa walikuwa na afya nzuri tangu ujana wao.
Unaweza kupata
mabadiliko na matatizo katika tendo la ndoa hata katika umri wa ujana au kabla
ya umri wa miaka sitini endapo utakuwa na matatizo mbalimbali ya kiafya.
Utafiti mwingine unaonyesha kuwa idadi kubwa ya matatizo haya hutokea katika
umri wa miaka 35 hadi 55, hii ni kwa wote wanaume na wanawake kutokana na
sababu mbalimbali.
MAGONJWA YA WAZEE
YANAYOATHIRI UFANYAJI WA TENDO LA NDOA
Wazee
kuanzia umri wa miaka sitini husumbuliwa na magonjwa mbalimbali kama
tutakavyoona.
Matumizi ya baadhi ya madawa kwa muda mrefu kutokana na matatizo
mbalimbali pia huwaathiri na endapo walishawahi kufanyiwa upasuaji katika
viungo vyao vya uzazi.
Matatizo
ya kimahusiano na mpenzi wako pia huweza kukuathiri.
Kwa hiyo matatizo haya
tunategemea tunayapata kwa wazee endapo utajikuta unapata matatizo haya na wewe
upo katika umri wa chini ya miaka sitini basi ujue mwili wako unaanza kuchoka
na unatakiwa ufanyiwe uchunguzi wa kina.
Magonjwa ya wazee yanayoathiri uwezo
wa kufanya tendo la ndo ni kama vile: Arthritis: Ni maumivu ya mifupa mwilini
katika sehemu za maungio, hasa magoti, viwiko vya mikono, mabega, kiuno na
mgongo.
Ni vema wazee wawe na tabia ya kufanya mazoezi kidogokidogo, kupumzika
na kila wakati wanapooga waoge maji ya uvuguvugu. Ni vizuri wapate tiba kwa
matatizo hayo.
Itaendelea wiki ijayo
DK. CHALE SIMU:
+255713350084.
|
No comments:
Post a Comment