
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, kiwango cha ubora na usalama wa dawa nchini kimeongezeka kwa zaidi ya asilimia 95.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti Sillo, amemweleza
mwandishi wetu hivi karibuni kuwa kwa sasa usalama wa dawa nchini
umeongezeka na kwamba Taasisi yake imejizatiti kuongeza weledi wa
udhibiti.
“Hivi
sasa udhibiti ni mkubwa hivyo dawa zetu ni salama kwa kiwango cha kati
ya asilimia 92.5 hadi asilimia 98,” alisema Bw. Sillo.
Aliongeza
kuwa hivi sasa hali ya soko la dawa ni salama na taasisi yake
inafuatilia kwa karibu ubora na usalama wa dawa kwa kutumia mfumo maalum
wa ukaguzi.
Bw.
Sillo aliongeza kuwa, mafanikio hayo yanatokana na kuimarika kwa uwezo
wa taasisi yake pamoja na ushirikiano mkubwa kati ya taasisi yake na
wadau wakiwemo wananchi.
Mkurugenzi
Mkuu huyo, alibainisha kuwa taasisi yake imeongeza uwezo wake kwa
kuajiri watumishi hadi kufikia zaidi ya 300 kutoka watumishi 53
ilipoanzishwa. Aidha, mbali ya kufungua ofisi za kanda saba (07), TFDA
imeongeza uwezo wa maabara zake za uchunguzi na zimepata ithibati za
umahiri za kimataifa ikiwa ni pamoja na kutambuliwa na Shirika la Afya
la Dunia (WHO).
“Uwezo
wetu umekuwa mkubwa na tuko karibu na maeneo yote ya udhibiti. Hivi
sasa mbali ya ofisi zetu za kanda, lakini pia tuna wawakilishi katika
kila Halmashauri nchini,” alisema.
Alifafanua
kuwa Halmashauri zote zina wataalamu ambao wanafanya kazi kwa niaba ya
Mamlaka ambapo wanasimamia na kudhibiti ubora na usalama wa dawa kwa
kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa maelekezo ya TFDA.
Hivi
sasa TFDA ina ofisi za kanda saba ambazo ni Kanda ya Ziwa, Kanda ya
Kati, Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Magharibi, Kanda ya Mashariki, Kanda
ya Kusini na ya Nyanda za Juu Kusini.
Mkurugenzi
Mkuu huyo aliwapongeza wataalamu wa taasisi yake kwa kazi nzuri
wanayoifanya na kuwashukuru wadau mbali mbali kwa ushirikiano wao na
hasa wananchi ambao amesema wamekuwa mstari wa mbele kushirikiana na
taasisi yake kutoa taarifa zinazohusu uvunjifu wa sheria.
Kwa mujibu wa takwimu zilizopo, katika kipindi cha mwaka 2003 hadi Juni, 2017, TFDA imesajili dawa 12,474.
Kwa
upande wa dawa zilizoingizwa na kugundulika kuwa hazina ubora, katika
kipindi hicho, TFDA iliteketeza dawa zenye jumla ya thamani Shilingi
bilioni 11.591.
Na Mwandishi Wetu, MAELEZO





No comments:
Post a Comment