|
Obadia
Frank alipofikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.
MKAZI wa
Chato mkoani Geita, Obadia Frank (41), mapema leo amefikishwa katika
mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kuchapisha taarifa za uongo
kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook kuhusu mazungumzo kati ya Serikali na
wawakilishi wa kampuni ya Acacia.
Akisomewa
hati ya mashtaka na wakili wa serikali, Leonard Challo, amedai mshtakiwa huyo
ambaye ni wakala wa Bayport ametenda kosa hilo Agosti 8 mwaka huu,2017 katika
Wilaya ya Chato mkoani Geita.
Imedaiwa
mbele ya Hakimu Mkazi, Wilbard Mashauri, kuwa siku hiyo mshtakiwa alichapisha
taarifa kupitia ukurasa wake wa Facebook uliokuwa ukihusiana na mazungumzo kati
ya serikali na kampuni ya Acacia.
Mshtakiwa
huyo anadaiwa kusambaza maneno kuwa “Taarifa kutoka kikao cha
mazungumzo kati ya Serikali na wawakilishi wa kampuni ya Acacia kuwa wanasheria
wa upande wetu wanashindwa kutafsiri baadhi ya vifungu vya sheria hadi kufikia
kuomba msaada kwa wanasheria wa Acacia sasa huoni hivi ni vituko mwizi
anakusaidia sheria haahaa haha.”
Inadaiwa
aliendelea kusambaza maneno kuwa, “mazungumzo bado yanaendelea lakini
wanasheria wetu wamebanwa sana ukizingatia wale jamaa wana vielelezo vyote vya
mikataba kiukweli tumuombe Mungu maana Serikali ikitaka kuvunja mkataba na
Acacia gharama kubwa zitatuusu.”
“Lakini
pia kuendeleza uvyama utatugharimu saana, baada ya mh. Rais Magufuli
angewashirikisha mawakili wasomi waliokwishaiva wakili Lissu, wakili Kibatara
na Fatma Karume kwenye mambo ya umuhimu kama haya yeye kaleta uchama sasa
itatugharimu .// Dicteta Magufuli mist go”. Maneno hayo yanadaiwa kusambazwa na
mshtakiwa huyo kupitia mtandao huo wa kijamii wa Facebook.
Imedaiwa
mshitakiwa ametenda hayo huku akijua kuwa taarifa hizo ni uongo na zilikuwa na
nia ya kuipotosha jamii.
Hata hivyo
mshtakiwa huyo anayetetewa na wakili Peter Kibatala, amekana kutenda kosa hilo
na amerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti na kesi hiyo
itatajwa Oktoba 16 mwaka huu,2017.
Mahakama
imemtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika ambao walitakiwa
kuweka bondi ya Sh. milioni tano.
NA DENIS
MTIMA/GPL
|
No comments:
Post a Comment