|
Mhasibu wa
Shule ya Sekondari ya Mtakatifu Joseph, Elizabeth Asenga (40) amehukumiwa
kulipa faini ya Sh 5 milioni ama kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela baada
ya kukutwa na hatia katika shitaka la kutuma ujumbe wa kumkashifu
Rais John Magufuli kupitia mtandao wa WhatsApp.
Hakimu Mkazi
Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Huruma Shaidi, ametoa hukumu hiyo leo Jumanne baada
ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi saba wa upande wa mashtaka na
utetezi uliotolewa na mshtakiwa mwenyewe na kumhukumu mshtakiwa huyo kulipa
faini ya Sh 5 milioni ama kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela.
Hata hivyo,
mshtakiwa huyo alifanikiwa kulipa kiasi hicho cha fedha na kukwepa adhabu ya
kifungo.
Kesi hiyo
namba 317 ya 2016 mshtakiwa huyo alidaiwa kuwa Agosti 6, 2016, aliwasilisha
ujumbe wenye mazingira ya kumkashifu Rais Magufuli kwa njia ya WhatsApp kwenye
kundi la kijamii liitwalo STJ Staff Social Group.
Mshtakiwa
huyo aliandika ujumbe usemao: ‘Godmorning humu. hakuna Rais kilaza kama huyu
wetu duniani, angalia anavyompa Lissu umashuhuri, fala lile, picha yake
ukiiweka ofisini ni nuksi tupu.
Ukiamka asubuhi, ukikutana na picha yake ya
kwanza siku inakuwa mkosi mwanzo mwisho.”
Baada ya
kusomewa shitaka hilo alikana na alikuwa nje kwa dhamana kwa kuwa na
wadhamini wawili ambao kila mmoja wao alisaini hati ya dhamana ya maneno ya Sh
2 milioni.
|
No comments:
Post a Comment