![]() |
|
Mwl God
Gwabunga kushoto ( mwenye koti jekundu) akipokea Saruji toka kwa Bw.Hilali
Ruhundwa ( mwenye fulana nyeupe).
Ameongeza
kuwa licha ya shule hiyo kuwa pembezoni mwa nchi lakini inafanya vizuri
kitaaluma kuliko hata shule zilizopo jijini Dar es Salaam.
"Makao
makuu ya kampuni yetu yapo Dar es Salaam na tungeweza kusaidia kule lakini wao
wana uwanda mpana wa kupata wadau wa maendeleo ikilinganishwa na huku Ngara
ambapo ni pembezoni mwa nchi". Ameongeza.
Akipokea
mchango huo, mwalimu wa taaluma wa shule hiyo Bw. God Marco Gwabunga , licha
ya kuishukuru kampuni ya Wazalendo kwa mchango huo, amewaomba wadau wengine wa
maendeleo hasa wazawa wa wilaya ya Ngara wanaoishi nje ya wilaya hiyo kuwa na
moyo wa kuchangia maendeleo nyumbani kwao.
Gwabunga
amesema kuwa licha ya shule yake kufanya vizuri kitaaluma na kuongoza mkoa wa
Kagera kwa shule za msingi, bado wanakabiliwa na changamoto ya kukamilisha
ujenzi wa majengo ya bweni.
"Wazazi
wengi toka sehemu mbalimbali nchini na nje ya nchi wanatamani kuleta watoto wao
kusoma hapa lakini inawawea vigumu kutokana na kukosa sehemu ya malazi."
Amesema mwalimu Gwabunga.
|

![]() |
|
Bweni linalojengwa
Shuleni Hapo.
Mwalimu
Gwabunga ameongeza kuwa wana uhaba wa vifaa hasa mifuko ya saruji 150, vitanda
80, magodoro 160, vifaa vya kuvuna na kuhifadhia maji kwa kuanzia ili wanafunzi
wanaotoka maeneo ya mbali wapate malazi.
"Mpaka sasa tumefikia
hatua nzuri katika ujenzi wa bweni na endapo wadau wangeweza kutuchangia japo
vifaa hivyo basi tungeweza kuanza na angalau wanafinzi 80."
Ameongeza.
Akielezea siri
ya mafanikio ya NAPS kufanya vizuri kitaaluma, Mwalimu wa Shule hiyo Raban
Kijanjali amesema kuwa watoto si tu wanaandaliwa kitaaluma bali huandaliwa
kiroho pia ili kuwajengea nguvu ya Mungu pindi wanapokuwa masomoni.
"Shule yetu ipo chini
ya kanisa Anglikana hivyo wanafunzi wanalelewa kiroho na kimaadili jambo
linalochangia kuwaongezea nguvu katika masomo yao sanjari na tabia njema
shuleni na wawapo nyimbani. Kiukweli kila mzazi anayependa mtoto wake kupata
elimu na malezi bora anatamani kumleta mwanae NAPS lakini tumekwama ujenzi wa
mabweni". Amesema Kijanjali.
|
![]() |
|
Mchango huo
kutoka kampuni ya Wazalendo, ni matokeo ya utekelezaji wa ahadi aliyotoa Bwana
Ruhundwa wakati wa mahafali ya darasa la saba yaliyofanyikia shuleni hapo hivi
karibuni.
Wazalendo ni
kampuni inayojishughulisha na shughuli mbalimbali hasa kuandaa matamasha, kuzalisha na kusambaza simulizi na vipindi
vya TV na Radio, kupokea na kutembeza watalii, mavazi na fashion n.k.
NAPS ni
shule inayomilikiwa na kanisa Anglikana Dayosisi ya Kagera ambayo imekuwa
ikifanya vizuri kitaaluma mkoani Kagera.
Shule hii
inasifika pia kwa kuwa na gharama ndogo sana ya ada.
|









No comments:
Post a Comment