![]() |
|
Mfalme
Mswati wa Tatu wa Swaziland akikagua Gwaride.
|
![]() |
|
Mfalme
Mswati III na mkewe mpya.
Mfalme
Mswati wa Tatu wa Swaziland kwa mara nyingine ameongeza idadi ya Wanawake kwa
kuoa mwanamke mwingine.
Katika kuadhimisha Ngoma ya Umhlanga ambayo hufanyika
kila mwaka kwa kumpa mfalme fursa ya kuchagua mwanamke wa kuoa, mfalme huyo
hivi karibuni alimchagua Siphele Mashwama mwenye umri wa miaka 19 kuwa mkewe wa
14.
|
![]() |
|
Wakiwa
kwenye sherehe za mwaka.
Msichana
huyo ambaye ni binti wa Waziri Jabulile Mashwama katika Serikali ya nchi hiyo,
alipewa manyoya maalum mekundu ya ndege anayejulikana kama emagwalagwala ambaye
huhusishwa na sherehe hiyo maalum ya kifalme.
Mswati ambaye ana umri wa miaka
49 huchagua wanawake waliovuka umri wa miaka 19.
|
![]() |
|
Wakiwa
kwenye sherehe za mavuno.
Pamoja na
talaka kupigwa marufuku katika nchi hiyo ya kifalme, Mfalme Mswati amewahi
kuwataliki wake zake watatu.
Siphele ambaye ni mhitimu wa Waterford Kamhlaba
World University College, alifuatana na Mfalme Mswati alipohudhuria Mkutano
Mkuu wa Umoja wa Mataifa hivi karibuni.
Habari hiyo
ilifichuliwa na msimamizi wa sherehe za kifalme, Hlangabeza Mdluli,
aliyethibitisha kwamba Mswati alikuwa amefuatana na mkewe huyo ambaye kwa umri
ndiye mdogo zaidi.
|
![]() |
|
Wake
wengine wa Mswati.
Wake zake
wengine ni pamoja na: Inkhosikati LaMatsebula, Inkhosikati LaMotsa, Inkhosikati
LaMbikiza, Inkhosikati LaNgangaza, Inkosikati LaMagwaza (ameachika),
Inkhosikati LaHoala (ameachika), Inkhosikati LaMasango, Inkhosikati LaGija
(ameachika).
|
![]() |
|
Wakiwa
kwenye sherehe za mwaka.
Wengine ni:
Inkhosikati Magongo, Inkhosikati LaMahlangu, Inkhosikati LaNtentesa, Inkhosikati
LaNkambule, Inkhosikati Ladube na Inkhosikati LaFogiyane. Mfalme King Mswati,
anayejulikana pia kama Ngwenyama, yaani simba, anasemekana kuwa na watoto zaidi
ya 13 ambao ni pamoja na binti yake mkubwa zaidi aitwaye Sikhanyiso, Sibahle
Dlamini, Makhosothando Dlamini, Majaha Dlamini, na Tiyandza Dlamini.
Wengine ni
Sakhizwe Dlamini, Saziwangaye Dlamini, Bandzile Dlamini, Lindaninkosi Dlamini,
Mcwasho Dlamini, Temtsimba Dlamini na Temaswati Dlamini.
Baba
yake Mswati, Mfalme Sobhuza wa Pili, alioa wanawake 70. Mswati amekuwa
akishutumiwa kwa kujilimbikizia utajiri wakati watu wake wengi ni maskini.
Hivi
karibuni, Nchi hiyo ndogo ilitumia kiasi cha Dola milioni 2.2 (sawa na Sh.
bilioni 5) kwa kununua magari ya anasa aina ya BMW 740i na pikipiki 80.
Magari
hayo yalikuwa ni kwa ajili ya viongozi wa Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa
Afrikca (SADC) waliyoyatumia kwa ajili ya mkutano wa siku mbili.
|











No comments:
Post a Comment