![]() |
|
Makamu wa
Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) na Askofu wa Jimbo Katoliki la Ngara, Kanisa Katoliki Ngara,
Severin Niwemugizi.
Askofu wa
Kanisa Katoliki Ngara, Severin Niwemugizi amesema yuko tayari kuitwa mchochezi
endapo kundi la watetezi wa haki za binadamu watachukuliwa kama wachochezi.
Askofu
Niwemugiza amesema yeye kama kiongozi wa dini anaongozwa na maadili, haki na
ukweli hivyo hajali namna wengine watakavyomchukulia.
Akifungua
mkutano wa asasi za kiraia uliolenga kujadili kuhusu Katiba Mpya leo Jumatano,
Askofu Niwemugizi amesema imefika wakati nchi inahitaji kuwa na dira nzuri.
Amesema
hakuna mtetezi wa haki za binadamu anayetaka nchi iingie kwenye machafuko kwani
wote lengo lao ni kuchochea maendeleo, amani na utulivu.
Askofu Niwemugizi
amesema kuanza kutokea kwa matukio ya kuteka watoto, vifo katika mazingira ya
kutatanisha na ongezeko la watu wasiojulikana ni ishara mbaya.
“Hizi sio
dalili nzuri kwa Taifa lenye afya njema. Ni vielelezo vyenye dira mbaya.
Imefika wakati tukae kama Taifa tukubaliane kuwa tunataka dira njema ambayo ni
Katiba.”
Amesema
anatambua jitihada anazofanya Rais John Magufuli katika kupambana na ufisadi na
kutaka rasilimali ziwanufaishe wanyonge lakini ni muhimu juhudi hizo zilindwe
na Katiba nzuri.
“Rais
anafanya mengi mazuri na alipoanza kila mmoja aliona dalili za matumaini lakini
juhudi hizo zinaweza zisiwe endelevu kama hakuna ulinzi wa Katiba,”
“Tunahitaji
Katiba tena Katiba nzuri ambayo haitaruhusu kuchezewa na yeyote kwa maslahi au
matakwa yake binafsi.”
Amesema,
“Namshauri Rais achunguze kwa makini yatakayozungumzwa kwenye mkutano huu, ayaone kuwa yana nia njema na ayafanyie
kazi.”
SOURCE: Mwananchi.
|
Wednesday, September 27, 2017
Askofu Niwemugizi Aamua Kukubali Kuitwa Mchochezi
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.






No comments:
Post a Comment