|
Upelelezi wa
awali katika kesi ya utakatishaji fesha inayowakabili Rais wa Simba SC, Evans
Aveva na Makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ umekamilika katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu.
Wakili wa
Serikali, Nassoro Katuga amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa leo
September 18, 2017 kuwa, upelelezi wa awali wa kesi hiyo umekamilika ambapo
jalada la kesi limepelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ili alisome na
kueleza kama anaona umekamilika au la.
Baada ya
kuelezwa hayo, Hakimu Nongwa aliahirisha kesi hiyo hadi September 27, 2017.
Aveva na
Kaburu wanashtakiwa na TAKUKURU wakikabiliwa na tuhuma za kughushi nyaraka za
Klabu ya Simba na kutakatisha fedha kiasi cha dola za Marekani 300,000 (zaidi
ya Sh milioni 650) na wamekuwa rumande tangu Juni 29, mwaka huu.
Upelelezi
uliokuwa unafanyiwa kazi ni nyaraka za kughushi maandiko zilizokuwa zimepelekwa
kwa mtaalam kufanyiwa uchunguzi ili kubaini makosa hayo.
|
No comments:
Post a Comment