Taswira Picha -Walimu 26 wa michezo kutoka Shule 14 za msingi Ngara watunukiwa Vyeti na Shirika la Jambo Bukoba. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, September 18, 2017

Taswira Picha -Walimu 26 wa michezo kutoka Shule 14 za msingi Ngara watunukiwa Vyeti na Shirika la Jambo Bukoba.

September 16,2017 -Walimu 26 wa michezo kutoka Shule 14 za msingi za kata ya Kasulo,Rusumo na Nyakisasa wilayani Ngara mkoani Kagera wamehitimu mafunzo ya kuwajengea uwezo wa michezo mbalimbali kupitia stadi za maisha na kutunikiwa vyeti na kukabidhiwa vifaa vya michezo ikiwemo mpira mmoja kwa kila shule na kitabu cha mafunzo kutoka shirika lisilo la kiserikali la Jambo Bukoba la mkoani kagera linalojihusisha na elimu ya michezo kwa shule za msingi mkoani humo.
Kushoto ni Mmiliki wa Mtandao huu Mohamed Makonda aka Mwana wa Makonda katika pozi la picha na Mkurugenzi wa Jambo Bukoba mkoani Kagera Steven Gonzaga mara baada ya Mafunzo kufungwa katika Shule ya Msingi Njia Panda-Benaco.

Mafunzo hayo ambayo yamefanyika katika shule ya msingi Njia Panda ,kata ya Kasulo wilayani Ngara yamefungwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilkaya ya Ngara , Aidan Bahama na kuwaagiza Wakuu wote  Shule za Msingi pamoja na Walimu wao wa Michezo kuandaa mpango kazi utakaonesha namna michezo mbalimbali itakavyofundishwa na kuchezwa katika shule zao.

Hapa mchezo wa kumtambua kwa macho Mtu mwenye UKIMWI Ukichezwa na Washiriki ambapo mtu husimama mbele yao na kuambiwa amguse Mtu aliye na kijiti nyuma kama picha inavyoonesha .


Picha Juu na chini mchezo wa kuokota kijiti,kisha unakimbia na kwenda kuandika neneo UKIMWI UPO  ,unakuza Ubunifu,Kujiamini,Ushirikiano na Wepesi katika kukimbia.




Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera Aidan Bahama akikagua Maandishi ya Neno UKWIMI UPO  yaliyoandikwa na Washiriki wa mafunzo ya Jambo Bukoba wakati wa hafla ya kufungwa September 16,2017.



Pichani juu na chini Washiriki wakicheza mchezo wa kuunda umbo la pembe tatu kwa kutumia Kamba.


Kutoka kulia ni Steven Ngonzaga Mkurugenzi wa Shirika la Jambo Bukoba wakifurahia wimbo uliokuwa ukiimbwa wa Jambo Bukoba sambamba na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera Aidan Bahama , Pembeni yake ni Afisa Michezo wilaya Said Salumu na Mratibu Elimu Kata ya Kasulo.
Kulia ni Diwani wa Kata ya Kasulo Dr Philbert Kiiza akiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera Aidan Bahama Katikati na Mratibu Elimu kata hiyo kushoto.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika la Jambo Bukoba mkoani Kagera Steven Gonzaga Pichani, ametoa wito kwa Viongozi wa Kiserikali,Chama na Wadau wengineo  kuhakikisha wanahamasisha michezo inayofundishwa na Shirika hilo,inachezwa wakati wote mashuleni ili kutimiza lengo la Mafunzo ambayo yamekuwa yakitolewa kwa Walimu wa Michezo wa Shule za Msingi mkoani Kagera.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera Aidan Bahama akisoma kitabu cha Muongozo wa Mafunzo ya Jambo Bukoba wakati wa hafla ya kufungwa kwa Mafunzo Jumamosi September 16,2017 katika Shule ya Njia Panda ,Kata ya Kasulo wilayani Ngara.


 Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera Aidan Bahama akigawa Cheti kwa Mwalimu aliyehitimu Mafunzo..

Said Salumu ni Afisa Michezo wilaya ya Ngara na Philbert Kiiza , Diwani wa kata ya Kasulo wamesema kuwa baada ya Walimu hao wa Michezo  26 kutoka kata Kasulo,Rusumo na Nyakisasa kupata mafunzo hayo,watahakikisha wanawafatilia na kutoa ushirikiano wa kutosha ili kufikiwa mafanikio ya michezo mashuleni.

Nao Walimu waliozungumza na Mtandao huu wameahidi kuwa mabalozi wazuri mashuleni kwako kwa kuandaa mpango kazi wa michezo utakaohakikisha Wanafunzi wanacheza michezo mbalimbali ili Kujenga na kukomaza afya ya mwili na akili;Kujenga ukakamavu, nidhamu na Kuonyesha uwezo na vipaji vya washiriki na Kukuza na kuendeleza uhusiano wa kirafiki baina ya Shule mbalimbali.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad