![]() |
|
Mkuu wa Mkoa
Arusha, Mrisho Gambo ametumia ukurasa wa Facebook kuwapa nguvu vijana na
kuwafariji juu ya mambo mbalimbali ambayo yanatokea katika maisha na kusema
kuwa vijana wengine wanaona hawawezi jambo fulani ni kutokana na kuwa na njia
mbadala.
Mrisho Gambo
amesema kuwa katika maisha ya kawaida siku ambayo mtu akifukuzwa kazi ndipo
anaweza kugundua kuwa anaweza kuishi maisha yake vizuri bila ya kuwa na hiyo
kazi na siku ambayo vijana wengine wanaweza kuanza kutumia vipaji vyao
watagundua kuwa wanaweza kuishi bila kutegemea vyeti vyao.
"Siku
utakayofukuzwa kazi utashangaa kuwa unaweza kuishi bila hiyo kazi, siku
utakayoanza kutumia kipaji chako utashangaa kuwa unaweza ishi bila Digrii yako,
siku Utakayoanza kutumia Ubunifu au Kutumia Taaluma yako utagundua kuwa unaweza
kuishi bila kutegemea kupandishwa cheo, mengi unayodhani huyawezi ni kwa sababu
tu una njia mbadala" alisema Mrisho Gambo
|







No comments:
Post a Comment