|
Ofisi ya
Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania -Dodoma imetoa taarifa kuhusu Mwenyekiti wa CHADEMA –Mhe.Freeman
Mbowe kunyang’anywa na Bunge gari lake alilokua analitumia kwenye shughuli
mbalimbali za kumuhudumia Tundu Lissu mjini Nairobi nchini Kenya.
Ofisi ya
Bunge imesema ililazimika gari hilo lirudishwe Tanzania na kuegeshwa kwenye
ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha kwa sababu
Dereva wake hakua amekamilisha taratibu za kiofisi kama inavyotakiwa hivyo sasa
hivi yuko Dodoma kuzikamilisha.
Awali CHADEMA
ilisema Mbowe ambaye ni Mbunge wa Hai, aliamuru gari hilo lipelekwe Nairobi kwa
ajili ya kusaidia matibabu ya Lissu ambaye ni Mwanasheria mkuu wa chama hicho.
Lissu ambaye
pia Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), alishambuliwa na kujeruhiwa
kwa risasi Septemba 7 akiwa nyumbani kwake Area D mjini Dodoma na yuko Nairobi
kwa matibabu.
|
No comments:
Post a Comment