|
Kamishna
Jenerali wa Uhamiaji nchini Dr Anna Peter Makakala akiwa wilayani Ngara,mkoani
Kagera September 27,2017 .Kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Ngara Luten Kanali
Michael Mtenjele.
Akiwa wilayani
Ngara, Kamishina
Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Dkt. Anna P. Makakala amewataka wananchi wa
Wilaya hiyo kushirikiana na idara ya uhamiaji ili kuwabaini na kudhibiti
wahamiaji haramu wanaoingia nchini kupitia vijiji vya Wilaya hiyo.
Pia ameita Kamati
za Ulinzi na Usalama katika wilaya ya Ngara, Misenyi ,Karagwe na Kyerwa
mkoani Kagera kusitisha kupokea
wakimbizi katika kambi za muda kwa raia wanaotoka nchi jirani na
na kwamba nchi wanakotoka wakimbizi hao kuna amani na utulivu hivyo
warejee na kujenga nchi yao kimaendeleo
na kiuchumi.
|
No comments:
Post a Comment