![]() |
|
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Dkt John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoanza leo
Jumatano ya Septemba 27, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Matokeo
yake, usiri huo uliibua ubashiri ulioenezwa katika mitandao ya kijamii kuwa
wabunge wachache ambao wamekuwa wakionekana kuikosoa Serikali, wamevuliwa
uanachama.
Hata hivyo, haijathibitisha habari hizo.
Picha
zilizotumwa na Ikulu jana zinaonyesha wajumbe wa kamati hiyo wakiwa wamesimama
kabla ya kuanza kikao, bila ya kuwapo Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Picha moja inamuonyesha Rais Magufuli akiingia kikaoni, akiwa ameongozana na
naibu katibu mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo ambaye anaonekana kuwa ndiye
aliyeshika nafasi ya Kinana.
|
![]() |
|
Rais
Magufuli akisalimiana na wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM baada ya kumaliza mkutano
uliofanyika jana jijini Dar.
Picha na Ikulu.
Mpogolo pia
anaonekana pembeni ya Magufuli ndani ya kikao kuthibitisha kuwa alishika nafasi
ya Kinana sehemu fulani ya kikao hicho.
Hakuna taarifa zilizotolewa kuhusu kutokuwepo
kwa mtendaji huyo mkuu wa CCM na kama aliingia kikaoni baadaye. Picha nyingine
inamuonyesha Waziri Mkuu wa zamani, Salim Ahmed Salim, ambaye huenda
alikaribishwa kuhudhuria kikao hicho.
Salim na
marais wa awamu tatu zilizotangulia kabla ya Serikali ya Jakaya Kikwete, ndiyo
waliofanya kazi kubwa ya kutuliza wajumbe wa Halmashauri Kuu mwaka 2015 wakati
zogo lilipoibuka kutokana na jina la Edward Lowassa kuenguliwa na Kamati Kuu
kuwania kugombea urais kwa tiketi ya CCM.
Habari
ambazo zilizipatikana jana zilieleza kuwa Kamati Kuu ilianza kwa kupokea
taarifa ya Kamati ya Maadili kuhusu mwenendo wa wagombea wakati wa mchakato wa
kuchukua fomu hadi sasa.
Taarifa hiyo
ndiyo inayotumiwa na Kamati Kuu kupitisha au kuondoa wagombea, ambao
hawakuruhusiwa kujitangaza, kujipitisha kwa wapigakura wala kutumia mbinu
nyingine yoyote kutafuta kura hadi watakapotambulishwa mbele ya wapigakura.
|
![]() |
|
Makamu
wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Zanzibar, Mohammed
Shein.
Pia ripoti
hiyo itawaweka bayana wanachama ambao wamesukumwa na watu wenye fedha ili
wawatumie kwa malengo binafsi baadaye.
Pia, taarifa zinasema mchujo huo
utawagusa wale waliotahadharishwa kugombea kutokana na vitendo vyao vya
ukiukwaji wa maadili ndani ya chama.
Taarifa
zinaeleza kuwa licha ya kuweka miiko ya kugombea uongozi ndani ya chama, kama
kuwakataza watumishi wa Serikali kugombea nafasi ambazo baadaye zitawalazimu
kusimama kwenye majukwaa ya kisiasa kunadi sera za chama, bado baadhi
walijitokeza kugombea na kupitishwa na vikao vya ngazi za chini.
Kikao hicho
pia kinaangalia maadili ya walioomba kugombea ili kuepuka kupitisha wagombea
ambao ni watuhumiwa wa ubadhirifu wa mali za chama, wasio wakazi wa maeneo
husika na waliopitishwa baada ya wengine kuonewa katika uteuzi na kuwapo
mgombea mmoja pekee aliyepitishwa badala kuwa na ushindani.
|









No comments:
Post a Comment