![]() |
|
Katika picha
hii iliyotolewa Ijumaa, watoto wanaonekana wakicheza katika Mto Chari katika
mji mkuu wa Chad, N'Djamena.
|
![]() |
|
Wafuasi wa
kiongozi mkuu wa upinzani Isaias Samakuva, wanaonekana wakuwa na jogoo mweusi,
nembo ya chama cha Unita chake Samakuva ambapo katika mji mkuu wa Angola,
Luanda, wafuasi wa chama tawala cha MPLA wanaonekana wakiwa na furaha katika
mkutano wa kampeni. Mgombea wa chama hicho Joao Lourenco anatarajiwa kuwa rais
baada ya Jose Eduardo dos Santos kutangaza atastaafu baada ya kuongoza wka
miaka 38.
|
![]() |
|
Katika mji
mkuu wa Ghana, Accra, mwanamke huyu alikuwa amevalia mahsusi kuhudhuria Tamasha
ya Sanaa ya Barabarani ya Chale Wote.
|
![]() |
|
Mamia ya
wasanii wenyeji na kutoka nje ya nchi walihudhuria tamasha hiyo siku ya
Jumamosi ambapo waliwatumbuiza waliohudhuria kwa sarakasi, vichekesho, kucheza
ngoma na mengine mengi.
|
![]() |
|
Hayo
yakijiri, nchini kenya wafuasi wa kiongozi mkuu wa upinzani Raila Odinga
waliandamana Nairobi siku ya Ijumaa. Upinzani umewatuhumu polisi kwa kutumia
nguvu kupita kiasi kukabiliana na waandamanaji walioandamana kupinga matokeo ya
uchaguzi mkuu wa tarehe 8 Agosti. Polisi wamekanusha tuhuma hizo.
|
![]() |
|
Jumamosi,
rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, 74, alilakiwa na baadhi ya magavana wa
majimbo ya nchi hiyo katika uwanja mkuu wa Abuja baada yake kurejea kutoka Uingereza
alikokuwa anapokea matibabu kwa miezi mitatu.
|











No comments:
Post a Comment