![]() |
|
Mwandishi wa
mtandao huu ametembelea maeneo yaliyoathirika na kuzungumza na wananchi
walioguswa na hali hiyo katika kata za Mubunda, Buganguzi na Ibuga, ambapo
wameeleza kuwa mvua hiyo ilinyesha ghafla muda wa mchana na kusababisha athari
hizo, huku watoto wakiogopa na kukimbia hovyo kutokana na hofu ya kuona migomba
ikianguka na nyumba zao.
Miongoni mwa
miundombinu iliyoharibika ni pamoja na shule ya Mkembe Sekondari ambayo darasa
zima zimeezuliwa na upepo.
|
![]() |
|
Aidha
wamesema kuwa wameweza kushirikiana na majirani zao ambao hawajaguswa na
dhahama hiyo kwa kuwapatia hifadhi ya muda, wakati wakisubiri kuangalia jinsi
ya kurudishia hali zao.
Wametumia
nafasi hiyo kuiomba serikali kuwasaidia kwa muda walau chakula la malazi,
katika kipindi ambacho wanaendelea na mchakato wa kurudishi mazingira yao.
Itakumbukwa
kuwa mwezi mmoja uliopita, mtu mmoja alifariki dunia kwa kula chakula
kilichosadikiwa kuwa na sumu katika kata hizo, na kusababisha watu wengine
zaidi ya 80 kulazwa kwenye hospitali, vituo vya afya na zahanati wilayani humo.
|







No comments:
Post a Comment