![]() |
|
Baadhi ya
Wakimbizi raia wa Congo wakiwa kwenye kambi ya muda ya Bugarama ,wilayani Ngara
mkoani Kagera wakiwa wamepoteza sifa ya ukimbizi wao kwa kukiuka taratibu za
kikimbizi.
|

![]() |
|
Kamishna Jenerali wa uhamiaji nchini Dr Anna
Peter Makakala akiwa wilayani Ngara,mkoani Kagera leo September 27,2017.
Kamati
za Ulinzi na Usalama katika wilaya ya Ngara, Misenyi ,Karagwe na Kyerwa
mkoani Kagera zimeagizwa kusitisha
kupokea wakimbizi katika kambi za muda kwa raia wanaotoka nchi jirani na
kwamba wageni watakaoingia sio wakimbizi watakuwa ni wahamiaji haramu.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dr Anna
Peter Makakala alitoa agizo hilo kwa nyakati tofauti katika ziara ya kiutendaji
mkoani Kagera leo September 27,2017 na kwamba nchi wanakotoka wakimbizi hao
kuna amani na utulivu hivyo warejee na kujenga nchi yao kimaendeleo na kiuchumi.
Dr Makakala amesema katika mkoa wa Kagera
unapakana na nchi ya Uganda Rwanda Burundi wananchi wasioe wanawake raia wa
kigeni kinyume na taratibu lazima
walipiwe hati ya ukaazi ambayo ni kiasi cha Sh 100,000 zinazolipiwa kupitia
idara ya uhamiaji wala si kuwapatia viongozi katika serikali za vijiji.
"Fedha hizo zinalipwa kwa kipindi cha
miaka miwili mara baada ya kukamilika mhusika anatakiwa alipie tena hivyo kuweni
makini kufuata taratibu" Alisema Dr Makakala
|
![]() |
|
Alisema wakimbizi wanaotoka nchini Burundi
wanatakiwa kurejea kwenye nchi yaokufanya shughuli za maendeleo na wasipokelewe kwenye kambi za muda zilizopo
katika kata ya Bugarama na Murusagamba wilayani Ngara
Katika Kambi ya Bugarama wamekutwa raia 109
kutoka nchini Kongo DRC waliotoka kambi
za Burundi wakidai wamekimbia nchi yao kwa kukosa amani na katika kambi za
Burundi zinakabiliwa na uhaba wa chakula ambapo Kamishna Jenerali Makakala
amesema raia hao wamepoteza sifa ya kuwa wakimbizi
“Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na
idara ya uhamiaji ifanya taratibu za kuwarejesha hawa raia kwenye kambi zao
licha ya kutambua kuwa DRC bado wanakabiliwa na changamoto za usalama kisiasa”
|
![]() |
|
Akizungumza na wafanyakazi wa idara ya
uhamiaji mjini Ngara na Kabanga Dr Makakala aliwataka watumishi wa idara hiyo
kufanya kazi kwa uadilifu kwa kujiepusha na vitendo cha rushwa na kuhudumia
wananchi bila upendeleo huku akisisitiza ushirikiano na watendaji wa idara hiyo
kutoka nchi jirani.
Akiwa katika kituo cha forodha Kobero mpakani
mwa Tanzania na Burundi aliwataka
madereva wa magari wanaokwenda
nchi za jirani kuhakikisha wanatumia paspoti kuingia katika mataifa ya
kigeni kuepuka usumbufu unaoweza
kuwakumba katika shughuli zao.
Pia aliahidi kuongeza watumishi wa idara ya
uhamiaji mkoani Kagera na kwamba ataiomba serikali isaidie kutoa vifaa
vya kufanikisha utendaji kazi wa idara ya uhamiaji vikiwemo vyombo vya
usafiri kukabiliana na wimbi la kudhibiti wageni sehemu zote za mipakani kote
nchini.
|
![]() |
|
Naye
Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Ally Mtanda alisema kuanzia Januari
hadi Agosti mwaka huu,2017 Idara hiyo mkoani Kagera kwa kushirikiana na Jeshi la
Polisi imekamata raia wa kigeni 2,426
kutoka mataifa mbalimbali ambapo waliorudishwa katika mataifa yao ni 1,790.
Alisema pia takwimu za kitaifa ni kwamba raia
141,639 waliingia nchini kati ya hao watanzania ni 67, 318 na wageni ni 74,321 ambapo wageni waliotoka Tanzania kwenda mataifa ya nje
ni 139,091 kati ya hao watanzania ni
73,738 na raia wa kigeni ni 65,353 kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa
kisheria.
Awali Mkuu wa wilaya ya Ngara Luteni Kanali
Michael Mntenjele akitoa taarifa ya wilaya hiyo kuhusu raia wa kigeni wanaoingia wilayani
huno amesema wilaya hiyo inao waomba hifadhi 223 kutoka Burundi na DRC ambao
wanapokelewa katika kambi ya Rumasi wilayani Ngara
Alisema changamoto maeneo ya mipakayao wazi
na kutokuwepo askari wa kutosha kila mpaka kudhibiti RAIA wa kigeni ambao
huingia kifanya kazi kwa watanzania baadhi hupata makazi na wengine kuolewa
Pia alisema vigingi vya mipaka vilivyowekwa
tangu ukoloni na vingine vya mwaka 2014 chini ya rais jk na Nkurunziza
vinaingia kwenye mashamba ya wananchi na kwamba walioolewa au kuoa wanakabiliwa
na ukosefu wa fedha dola 50 za kulipia hati ya ufuasi.
Picha/Habari na -Shaban Ndyamukama.
|










No comments:
Post a Comment