|
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Pwani Kamishna Msaizidizi Jonathan Shanna Warioba, ametoa onyo
kali kwa wananchi wenye tabia za udhalilishaji kwa wanawake kuacha tabia hiyo
mara moja huku akisema kwamba udhalilishaji umesababisha kifo.
Kamanda
Shanna amelazimika kusema hayo hayo
wakati akitolea ufafanuzi juu ya tukio la mauaji ya mkazi wa Kijiji cha Vilabwa Wilaya ya Kisarawe Imma Habibu (
26).
Kwa mujibu
wa Shanna Marehemu aliuwawa juzi majira ya saa mbili asubuhi wakati walipokuwa
kijiweni na wenzake baada ya kutokea ugomvi kati yake na Ramadhani Habibu (23)
ambaye ni ndugu yake, baada ya mwanamke mmoja ambaye anadaiwa kuwa na maumbile
makubwa (makalio) kupita, mbele yao.
Alisema
baada ya mwanamke huyo kupita mbele yao walianza mabishano ambapo marehemu
alisema mwanamke huyo ana makalio makubwa na Ramadhani alisema ni makalio ya
kawaida sio makubwa.
Kamanda Shanna
alieleza kuwa baada ya mabishano hayo ndipo ulipozuka ugomvi hadi kufikia hatua
ya Ramadhani kumuua kaka yake kwa kumchoma kisu kifuani upande wa kuliana na
alifariki dunia akiwa njiani anapelekwa hosptali ya kisarawe.
Alisema
Jeshi la Polisi linamshikilia mtuhumiwa kwa kufanya mauaji hayo na kuwa
atafikishwa mahakamani mara moja na kuwa
amekubali kuwa amefanya mauaji hayo.
Kufuatia,tukio
hilo Kamanda Shanna aliendelea kutoa onyo kwa wananchi na vijana wanaoshinda vijiweni kuacha tabia ya
udhalilishaji hasa kwa wanawake na kuwa
kufanya hivyo ni kosa kisheria na kuwa kama kuna mtu aliyefanyiwa
vitendo vya namna hiyo atoe taarifa polisi na atafikishwa mahakamani.
"Wito
kwa wale wanaokiuka haki za binadamu kwa kumdhalilisha mtu waache mara moja,
mfano kisheria hata kumkonyeza mtu ni kosa la jinai hivyo unapaswa kufika
polisi, na tutamfuatilia kisha kumpeleka mahakamani" Kamanda Shana
amefafanua
Pia Kamanda
Shanna ametoa rai kwa wanawake kuvaa nguo zinazositiri maungo yao ili kuepusha
vishawishi na matamanio kwa wanaume
|
No comments:
Post a Comment