Picha ya Muonekano wa Kilele cha Mlima Oldoinyo Lengai - Arusha. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, September 30, 2017

Picha ya Muonekano wa Kilele cha Mlima Oldoinyo Lengai - Arusha.

Muonekano wa kilele cha mlima Oldoinyo Lengai uliopo Arusha. Mlima huu wenye urefu wa mita 3188, upo ndani ya bonde la Ufa sehemu ya Gregory kwenye ukanda wa Bonde la Ufa tawi la mashariki.

Mlima huu ni volcano iliyo hai, ukitazama hapo kileleni ndio tundu la mlipuko wa volcano hiyo ambayo mara ya mwisho ililipuka( kutoka ) mwaka 2011 na 2013.
Oldoinyo Lengai ndio mlima wa volcano pekee duniani ambao unatoa ' lava' aina ya Natrocarbonatite lava. 

Lava hii huufanya mlipo wake kuwa mweusi tofauti na volcano nyingine ambazo hutoa miale miyekundu .

Huo ndio upekee wa mlima huu ambao kwa tafsiri ya kimasai neno ' Oldoinyo Lengai ' ni mlima wa Mungu.  
 
Na-Samuel Samuel

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad