Mafunzo ya
elimu ya ufundi yananafasi kubwa ya kuongeza, kusaidia na kukuza ajira kwa vijana wanaosoma masomo
hayo kwenye vyuo vya ufundi kwa
kuajiriwa au kujitengenezea ajira wao wenyewe.
Kaimu katibu
mtendaji wa baraza la taifa elimu ya ufundi (NACTE), Dkt, Adolph Rutayuga
amesema hayo Jana September 28,2017 Jijini dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa warsha ya mradi wa
kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini yaliyoandaliwa na UNESCO.
Akizungumza
kwa niaba ya Katibu mkuu wizara ya elimu,sayansi na teknolojia, Dkt, Rutayuga
amesema nia kubwa ya mradi huo ni kuangalia ufundi unaumuhimu gani kwenye sekta
ya uchumi hasa unapozungumzia sekta ya uchumi wa viwanda.
Aidha
tunaangalia ubora wa mafunzo yanayotolewa kwenye elimu ya ufundi sababu kukiwa
na vyuo vingi ambavyo vinaendeshwa katika ubora usiotakiwa, wanafunzi wanaotoka
kwenye vyuo hivi hawatakuwa wazuri.
“Tunalenga
kujenga mazingira ya kutoa mafunzo bora kwenye elimu ya ufundi, elimu iliyobora
kwa kusapoti walimu wanaofundisha,miundombinu ya kujifunza na kufundishia na
pia kujaribu kuangalia mahusiano yaliyopo kati ya viwanda na soko la ajira kwa
kile kinachotolewa kwenye vyuo vya ufundi.
Ameongeza,kama
suala zima la mambo ya mitaala, linaweza kuboreshwa, na ile dhana potufu ya
kizamani iliyokuwepo kwamba kwamba Tivet ni kwa wale walioshindwa,inapaswa
iondoke, watu wajue kwamba mchango mkubwa kwenye uchumi unafanywa na hawa watu
kwenye sekta ya kati
“Malengo
makubwa ni kujaribu kuinua ubora wa mafunzo yanayotolewa na vyuo vya ufundi,
kuinua umuhimu mafunzo ya ufundi na
Jinsi inavyoweza kisaidia kwenye maendeleo ya kukuza uchumi,” amesema.
Naye, Kaimu
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO), Axel Plathe amesema warsha hiyo itajadili kwa undani
vitendo vya ufanisi, utekelezaji na jukumu la uwezo ambao kila wadau watafanya
katika mradi uliopendekezwa chini ya maeneo matatu umuhimu, ubora na mtazamo wa
elimu na ujuzi wa kiufundi.
“Elimu bora
kwa Afrika itatekelezwa kuanzia mwaka huu hadi 2021 kwa lengo la kukuza elimu
na ujuzi wa kitaaluma na mafunzo ambayo ni muhimu kwa mahitaji ya soko la ajira
na mahitaji ya watu binafsi na jamii”amesema Plathe.
Kaimu Mkuu wa Ofisi na
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO), Axel Plathe akizungumza washiriki wa warsha ya kuzindua Mradi wa
mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini yaliyoandaliwa na UNESCO
warsha hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam September 28,2017.

Kaimu Katibu Mtendaji
wa Baraza la Taifa elimu ya Ufundi (NACTE), Adolf Rutayuga akizungumza kwa
niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia wakati wa Warsha
hiyo iliyoandaliwa na Unesco ya kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini
jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washririki na
Meza kuu wakiwa katika warsha ya uzinduzi wa Mpangowa kuimarisha elimu na
mafunzo ya ufundi nchini katika warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam Jana September
28,2017.


Baadhi ya washririki wa
Warsha ya kuzindua mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini
jijini Dar es Salaam.



Baadhi ya washiriki
Warsha ya kuzindua mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini
katika warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam .
![]() |
|
Kaimu Mkuu wa Ofisi na
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO), Axel Plathe na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa elimu ya
Ufundi (NACTE), Adolf Lutayuga wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya kuzindua mpango
wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi
nchini warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam Jana September 28,2017.
|
![]() |
|
Mtoa maada akizungumza
na washiriki wa warsha ya kuzindua mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya
ufundi nchini warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam. (Picha na Avila
Kakingo,Globu ya Jamii.)
|







No comments:
Post a Comment