Waumini wa
dini ya Kiislamu waliohudhuria Swala ya Eid el Fitr na Baraza la Eid Kitaifa
kwenye msikiti wa Masjid Riadha mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro wakimsikiliza
Waziri Mkuu Bw. Kassim Majaliwa wakati akitoa nasaha za Eid, tarehe 26 Juni, 2017.
"Mimi
nasema kuanzia leo, yeyote atakayekamatwa akitorosha chakula kwenda nje ya
nchi, chakula hicho kitataifishwa na kupelekwa ghala la Taifa na gari lake tutalitaifisha
na litaishia Jeshi la Polisi. Tunafanya hayo kwa lengo la kuwalinda Watanzania
tusikumbwe na baa la njaa."
Bw Majaliwa amesema kumekuwa na wimbi kubwa la
usafirishaji wa chakula kwenda nje ya nchi bila kibali.
"Hilo
ni kosa kubwa kwa sababu litasababisha nchi yetu kupata baa la njaa huko
mbele," amesema.
Amesema
mipaka ya Tarakea, Holili, Mwanga, Horohoro, Siha, Namanga na Sirari imekuwa
inapitisha kiasi kikubwa cha mazao ya chakula kwenda nje ya nchi jambo ambalo
ni hatari sana.
"Hii ni
kwa sababu chakula cha ndani hakitoshelezi mahitaji. Kwa sababu nchi zote za
jirani hazina chakula cha kutosha. Tusipokuwa makini, tutabaki tunalia
njaa."
Kenya ni
moja ya nchi ambazo zinakabiliwa na uhaba wa mahindi.
Bw Majaliwa amewataka wafanyabiashara wa ndani,
wachukue mahindi kutoka maeneo yenye mavuno mengi na kuyapeleka kwenye sehemu
zenye mavuno kidogo.
"Watanzania
tushirikiane, kama ni biashara tutoe huku kwenye mavuno mengi na tuyapeleke
Shinyanga na Geita ambako wanayahitaji au tukanunue Sumbawanga na kuyapeleka
kwenye mikoa mingine yenye upungufu," alisisitiza.
|
Tuesday, June 27, 2017
Serikali ya Tanzania yapiga Marufuku Usafirisha Chakula nje ya Nchi.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment