Saida Karoli.
Msanii
mkongwe wa muziki wa asili, Saida Karoli amewamiminia sifa kibao wasanii wa
Bongo Fleva, Ray C na Darassa.
Saida ambaye
kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya Orugambo, amesema hit song ya
Darassa ‘Muziki’ ni vigumu kuja kushuka na kuwataka wasanii wengine hasa wa hip
hop kuchukulia hilo kama somo.
“Wimbo wa
Darassa utaendelea kuhit, utaendelea kuwa shule kwa waimbaji wa hip hop.
Nitapenda watumie akili alizotumia Darassa, mimi naamini wimbo wa Darassa
hauwezi kushuka hata siku moja na Watanzania wengi walikuwa hawapendi muziki wa
hip hop lakini Darassa kuonyesha njia kwa sababu sasa hivi hadi kwenye harusi
wanaimba acha maneno weka muziki, hadi Bungeni,” amesema Saida.
Kwa upande
wa Ray C Saida amesema licha ya msanii huyo kupitia matatizo mengi bado uwezo
wake upo pale pale na kuna baadhi wamejaribu kumuiga ila wameshindwa.
“Kwa kweli
Ray C nampenda sana kutoka moyoni tangu zamani, sauti yake ni nzuri haina
mpinzania, wasichana wengi wamejaribu kuiga kuimba kama yeye, wanapenda mvuto
wake na muonekano wake lakini wameshindwa,” amesema Saida na kuongeza.
“Na
ukiangalia Ray C amepitia matatizo makubwa sana hapa katikati lakini napenda
kumshukuru Rais Mstaafu Mheshimiwa Jakaya Kikwete alipomsaidia Ray C, na
ningependa Rais wetu wa sasa, Dkt. John Magufuli afanye hivyo ili tuweze
kunyanyuka sisi tuliokwama,” ameeleza Saida.
|
No comments:
Post a Comment