Mwakilishi
wa Mashirika ya Kimataifa nchini na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Alavaro Rodriguez (katikati) akiwa
ameongozana na Mkurugenzi anayesimamia Mashirika ya Umoja wa Mataifa
,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Balozi
Celestine Mushi (kushoto) na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya
Weruweru ya mkoani Kilimanjaro,Rosalia Flavian wakiingia katika ukumbi
wa shule hiyo kwa ajili kongamano.
Wanafunzi
wa kidato cha Tano na Sita pamoja na wageni wakiimba wimbo kabla ya
kuanza kwa kongamano hilo lililolenga kuzungumzia juu ya Malengo ya
Maendeleo endelevu .
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Weruweru ,Rosalia Flavian akizungumza wakati wa Kongamano hilo.
Baadhi
ya Walimu katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Weruweru wakifuatilia
maelezo ya awali yaliyotolewa na Mkuu wa Shule hiyo.
Mkuu
wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Weruweru akiteta jambo na
Mwakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nchini na Mwakilishi Mkazi wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Alavaro Rodriguez.
Mwakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nchini na Mwakilishi Mkazi wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Alavaro Rodriguez akizunguza katika Kongamano hilo.
Baadhi ya wanafunzi katka shule ya Sekondari ya Wasichana ,Weruweru wakiwa katika kongamano hilo.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania ,Hoyce Temu akizungumza katika kongmano hilo.
Mkurugenzi anayesimamia Mashirika ya Umoja wa Mataifa ,Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Balozi Celestine Mushi akitoa
mada kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Weruweru juu
ya Malengo ya Maendeleo Endelevu .
Baadhi
ya Wananfunzi wa Shule ya Sekondari ,Weruweru wakiwa wameshikilia vibao
vinavyoonesha baadhi ya malengo mapya ya maendeleo endelevu wakati
Balozi Mushi akiwasilisha mada .
Balozi
Mushi akionesha Malengo mapya 17 ya Maendeleo Endelevu kwa wananfunzi
wa Shule ya sekondari Weruweru wakati akiwasilisha mada.
Balozi
Mushi akitoa zawadi ya Pesa kwa wanafunzi wawili wa kidato cha Tano na
Sita katika shule ya sekondari ya Wasichana ya Weruweru baada ya kuuliza
na kujibu vyema maswali .
Mwakilishi
wa Mashirika ya Kimataifa nchini na Mwakilishi Mkazi wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Alavaro Rodriguez akiwa
katika picha ya pamoja na walimu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya
Weruweru pamoja na wafanyakazi wengine wa Serikali.
Mwakilishi
wa Mashirika ya Kimataifa nchini na Mwakilishi Mkazi wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Alavaro Rodriguez akiwa
katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana
ya Weruweru.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
No comments:
Post a Comment