![](https://1.bp.blogspot.com/-PWl9g9Lcdwo/WKad0Vm0JAI/AAAAAAABBQA/C4oRPPYWaBIgufH7R8ogXWLjkjxQYyRtACLcB/s640/3.jpg)
![]() |
Mvuto
mwingine wa Mechi hii ni kupambanishwa kwa Mtu na Kaka yake Paul Pogba wa Man United na Kaka Mkubwa
Florentin Pogba Beki wa St-Etienne
ambae hakudumu Dakika 90 baada ya kuumia Dakika ya 79 na kubadilishwa huku
Mdogo Mtu akikosa Bao kadhaa na kupiga Posti pia.
Man United walifunga Bao lao la kwanza Dakika
ya 15 kwa Frikiki ya Zlatan Ibrahimovic
iliyombabatiza Mchezaji wa St-Etienne Pajot na kutinga.
Kipindi cha
Pili Zlatan Ibrahimovic alifunga Bao
nyingine 2 katika Dakika za 75 baada ya kazi njema ya Marcus Rashford na jingine Penati ya Dakika ya 88 baada ya yeye
mwenyewe kuangushwa kwenye boksi.
|
![]() |
Timu nyingine
ya Uingereza, ambayo iko EUROPA LEAGUE ni Tottenham
ambayo ilifungwa 1-0 na Klabu ya Belgium, Gent.
Nayo Klabu
ya Straika wa Tanzania, Mbwana Samatta,
Genk ya Belgium imetoka Sare 2-2 na Astra
Giurgiu ya Romania kwenye Mechi iliyochezwa huko Nchini Romania na Wenyeji
hao kunusurika kipigo kwa kusawazisha Dakika ya 90 kwa Bao la Takayuki Seto.
Kwenye Mechi
hiyo, ambayo Samatta alicheza Dakika zote 90, Genk walitangulia kufunga Dakika
ya 25 kwa Bao la Timoty Castagne 25 na Astra kusawazisha Dakika ya 43 kwa Goli
la Constantin Budescu 43.
Leandro
Trossard, Dakika ya 83, allipa Genk Bao la Pili.
Mechi za
Marudiano za Raundi ya Mtoano ya Timu 32 zitachezwa Alhamisi Februari 23,2017.
|
No comments:
Post a Comment