![]() |
Mke wa Rais
Mama Janeth Magufuli akisalimiana na mkuu wa mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi
alipowasili wilayani Manyoni mkoani Singida jana Februari 13, 2017.
|
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhYfaD3BDvfA_zdiYcYtXG3Dkz9dJsbCtIyH3FaIAf35q6QVDUY2gHJjJSDwv8hKUKAwFLvLIxXQNtxF_dQfD8tlHtbsrKp7Cu6_Znr0ZuxiKU80u0Dn9-1MXmir8Qb1HXHCx-OPgh-vdds/s640/2.jpg)
Mke wa Rais
Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakilakiwa kwa
furaha walipowasili katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya
Manyoni mkoani Singida jana Februari 13, 2017.
|
Afisa Ustawi
wa Jamii Yeremia Ngoo akiwapa maelezo Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke
wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa nyumbani kwa Bibi Agnes Kamota (75)
walipotembelea Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani
Singida jana Februari 13, 2017.
|
Mke wa Rais
Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiwa na Bibi
Agnes Kamota (75) walipomtembelea nyumbani kwake katika Makazi ya Wazee
Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida jana Februari 13, 2017.
|
ke wa Rais
Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakitembelea Zahanati ya Sukamahela katika Makazi ya Wazee
Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida jana Februari 13, 2017
|
![]() |
Mke wa
Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa akisalimia wananchi wakati yeye na Mke wa Rais
Mama Janeth Magufuli walipofanya ziara
katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani
Singida jana Februari 13, 2017.
|
Mke wa Rais
Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakishiriki
kucheza ngoma na vikundi vilivyojitokeza kuwalaki katika Makazi ya Wazee
Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida jana Februari 13, 2017.
|
Mke wa Rais
Mama Janeth Magufuli akihutubia wananchi wakati yeye na mke wa Waziri Mkuu Mama
Mary Majaliwa walipotembelea Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya
Manyoni mkoani Singida jana Februari 13, 2017.
|
Mke wa Rais
Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri
Mkuu Mama Mary Majaliwa wakioneshana kielele cha kilima cha Sukamahela ambapo
inasemekana ndipo ilipo alama ya kuonesha katikati ya nchi ya Tanzania wakati
wa ziara yao katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni
mkoani Singida jana Februari 13, 2017
|
Mke wa Rais
Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakitoa msaada wa
vyakula tani 7.5 katika Makazi ya Wazee
Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida jana Februari 13, 2017
|
Mke wa Rais
Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakipokea msaada
wa vyakula na vinywaji kutoka kwa Meneja wa tawi la Benki ya NMB Singida Bw. Abius
Mlengwa katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani
Singida jana Februari 13, 2017.
|
Mke wa Rais
Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakipokea msada
wa vyakula na vinywaji kutoka kwa Meneja wa Tawi la CRDB Manyoni Bw. Richard
Karatta katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani
Singida Jana Februari 13, 2017.
PICHA NA IKULU.
MKE wa Rais
Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli pamoja na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa
wametoa rai kwa Wanzania kujenga tabia ya kusaidia watu wasiojiweza na wenye
mahitaji maalumu.
Wake hao wa
viongozi pia wamewatahadharisha watumishi wanaofanya kazi katika vituo vya
kulelea wazee wasiojiweza wahakikishe misaada inayotolewa na wadau mbalimbali
inawafikia walengwa bila ya kuchakachuliwa.
Wameyasema
hayo (Jumatatu, Februari 13, 2017) wakati walipotembelea Makazi ya Wazee
wasiojiweza na walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma ya Sukamahela wilayani
Manyoni Mkoani Singida.
Katika kituo
hicho wamekabidhi tani 7.5 za vyakula mbalimbali ukiwemo mchele, unga wa sembe
na maharage, ambapo Mama Janeth amewataka viongozi wa kituo kuhakikisha chakula
hicho hakichakachuliwi.
Akizungumza
na wazee wa makaazi hayo, viongozi mbalimbali na wananchi wanaozunguka eneo
hilo Mama Janeth amesema “Naomba chakula hiki kitunzwe vizuri na hakikisheni
kinawafikia walengwa na kisichakachuliwe hii ni sadaka,”.
Kwa upande
wake Mama Mary amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza na kuwasaidia wazee
wanaoishi katika makaazi ya kulelea walemavu na wasiojiweza nchini kwa sababu
wanakabiliwa na changamoto nyingi.
“Watanzania
wote popote mlipo tukumbuke kutembelea vituo vya kulelea wazee kikiwepo na hiki
tulichokitembelea leo cha Sukamahela na kutoa misaada mbalimbali kkwa kadri
tutakavyojaaliwa,” amesema.
Awali Mkuu
wa Makazi hayo Bw. Yeremia Ngoo alisema kituo hicho kilianzishwa mwaka 1974
chini ya Idara ya Ustawi wa Jamii kwa lengo la kuwasaidia watu wenye ukoma na
wazee wasiojiweza mkoani Singida.
Bw. Ngoo
alisema kituo hicho chenye wakazi 62 kinakabiliwa na changamoto mbalimbali
ikiwemo ya upungufu wa wapishi ambapo kwa sasa yupo mmoja huku mahitaji yakiwa
ni wapishi wanne. Pia nyumba nyingi ni chakavu na zina nyufa.
Naye
Mwenyekiti wa Wazee waishio katika makaazi hayo, Mzee Andrea Yohana
aliwashikuru wake hao wa viongozi na kuwaomba waendelee na moyo huo wa kusaidia
watu wasiojiweza.
|
No comments:
Post a Comment