Kamanda wa
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro akizungumza na
wageni waliofika kwenye mkutano huo.
Mkutano
maalum wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na viongozi wengine
mbalimbali wa mkoa huo pamoja na waandishi wa habari, unafanyika Jana February 13,2017, kwenye Ukumbi
wa Mwalimu Nyerere, Posta jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine,
Makonda alikabidhi majina 97 ya
watuhumiwa wa madawa ya kulevya kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kupambana na
Dawa za Kulevya, Rogers Siang’a.
Akitoa
ripoti ya oparesheni ya kwanza na pili ya kusaka watuhumiwa wa dawa za kulevya, Kamanda Sirro, amesema;
“Taarifa ya
operesheni tuliyoifanya wiki ya tatu iliyozinduliwa na Mkuu wa Mkoa Paul
Makonda, lengo ni kuwakamata wote wanaojihusisha na biashara hii ya madawa ya
kulevya. Mkuu wa mkoa aliunda kamati ya kufanya upelelezi.
“Watuhumiwa
waliokamatwa ni 311 na vielelezo. Kete 544 za heroin, Mirungi bunda 21.
“Watuhumiwa
117 wamekutwa na vielelezo, 194 hawajakutwa na vielelezo.
“Watuhumiwa
77 walitakiwa kuja baada ya kutajwa na mkuu wa mkoa.
“Hadi jana
watuhumiwa 32 wameripoti na kuhojiwa, watuhumiwa 45 hawajaripoti na juhudi
zinafanyika kuwapata.” Kamnada Sirro alisema.
Kamanda
Sirro aliongeza kuwa, ambao hawajaripoti watasakwa popote walipo na kupelekwa
mahakamani.
“Watuhumiwa
wengine upelelezi unaendelea. Pongezi za dhati kwa mkuu wa mkoa kwa ushiriki
wake binafsi ya kuongoza mapambano haya. Ukishakuwa mwenyekiti wa kamati ya
ulinzi na usalama ni vizuri kwenda kwenye ground uone kazi zinazofanyika.
“Wote
waliotakiwa kufika kituo cha polisi na hawakufika, watatafutwa na watahojiwa,
hilo halikwepeki.
“Kuna
wengine wakubwa hawakuamini kama watalala mahabusu, ila walilala, tukikuhoji
hatukuachii sababu utaharibu utaratibu.
“Hakuna mtu
aliye juu ya sheria hata ukiwa na ukubwa kiasi gani. Nashukuru wengine wameanza
kujisalimisha wenyewe.” Alimalizia Sirro.
|
No comments:
Post a Comment