Mkuu wa mkoa
wa Dar es salaam Paul Makonda akimkabidhi kamishna wa kupambana na Madawa ya
kulevya Rogers Siyanga list ya majina 97 ya watuhumiwa wa biashara ya Madawa ya
kulevya.
Mkuu wa mkoa
wa Dar es salaam Paul Makonda amemkabidhi Kamishna mpya wa kupambana na Madawa
ya kulevya Rogers Sianga majina 97 ya watuhumiwa wa biashara ya Madawa ya
kulevya.
Aidha
watuhumiwa wawili kati ya hao, Chidi Mapenzi (mume wa Shamsa Ford) pamoja na
Ayub Mfaume wametakiwa kukamatwa leo.
Akizungumza
na waandishi Jumatatu hii ( February 13,2017) mbele ya Kamishna mpya huyo pamoja na viongozi
mbalimbali wa serikali, Makonda amedai katika list hiyo mpya wako watoto wa
viongozi wakubwa pamoja na vigogo wengine wakubwa wa ndani na nje ya nchi.
“Style yangu
ni kuwasema hadharani na haya majina 97 ninamkabidhi kamishna siyo kwamba mkoa
wa Dar es salaam tunatoka kwenye vita dhidi ya Madawa ya kulevya, sisi ndo moto
umekolea, tunamkabidhi yeye ili kupitia vyombo vyake anaweza kushughulika na
mtu yeyote aliyoko ndani na nje ya nchi.
Na hii list ambayo tumemkabidhi ni ya
wafanyabiashara wakubwa, na tutaendelea mpaka kwenye list ya saba, kwa hiyo leo
tupo kwenye list ya tatu lakini bado kuna list 4 mbele yetu,” alisema Makonda.
Aliongeza,
“Viongozi wa dini tunaomba mtuombee, kwa sababu kwenye kumbukumbu za nyuma
mlijatwa kwenye biashara ya Madawa ya kulevya, sitaona aibu kuwashughulikia,
Mungu utaratibu wake ni mzuri sana na sisi tutaendelea na mapambano mpaka
mwisho, kwa hiyo viongozi wa dini mnatakiwa kujiandaa kuna mambo ya kiuchunguzi
yanaendelea.
Kwahiyo sisi tumekukabidhi majina ya watu 97 na sisi tumebaki na
nakala,”
|
No comments:
Post a Comment