Mbali na timu zao kupata au kukosa Ubingwa wa taji la Mapinduzi, kuna wachezaji ambao wamejishindia zawadi/tuzo binafsi baada ya kumalizika kwa mashindano.
Tuzo zilizotolewa kwa wachezaji binafsi ni pamoja na;
Mfungaji bora – Simon Msuva (Yanga SC ) magoli 8
Mchezaji bora kijana/chipukizi – Said Mohamed ‘Messi wa Unguja’ (Taifa Jan’ombe)
Mchezaji bora wa mashindano – Method Mwanjale (Simba SC)
Golikipa bora wa mashindano – Aishi Manula (Azam FC hajaruhusu goli kwenye mechi tano za mashindano.
Mwamuzi bora wa mashindano – Mfaume Ali Narror
Kila mshindi wa tuzo binafsi amekabidhiwa kiasi cha shilingi milioni moja (1,000,0000) kama tuzo kutokana na umahiri waliouonesha kwenye mashindano ya mwaka 2017.
Agrey Morris (Azam FC) alitangazwa mchezaji bora wa mechi ya fainali. Mdau wa soka Raza Lee akamkabidhi viatu vya kuchezea mpira pamoja na kombe dogo kama tuzo kwa kufanikiwa kuwa man of the match.
Kuanzia hatua ya nusu fainali, Raza Lee alikuwa anatoa zawadi ya viatu kwa mchezaji anayetangazwa kuwa man of the match.
|
Saturday, January 14, 2017
Tuzo binafsi walizoshinda Wachezaji Mapinduzi Cup 2017.
Tags
# MATUKIO
# MICHEZO
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment