Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Ijumaa Januari
13,2017 amefungua rasmi viwanda viwili mkoani Shinyanga.
Rais
Magufuli amefungua Kiwanda cha kutengeneza vifungashio vya bidhaa mbalimbali
ikiwemo mifuko ya Sandarusi cha Fresho Investment Company Limited na kiwanda
cha Jambo Food Products Company Limited kinachojihusisha na uzalishaji wa
vinywaji baridi ikiwemo soda,juisi na maji.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameyaonya magazeti
mawili yanayoandika habari za uchochezi na kupotosha wananchi kwa kuwa
vinahatarisha amani ya nchini.
Ametoa onyo
hilo jana wakati akikagua na kufungua Kiwanda cha Jambo cha kuzalisha vinywaji
baridi mkoani Shinyanga.
Rais
Magufuli alisema Serikali haitayavumilia magazeti hayo mawili kwa kuandika
habari za uchochezi ambazo zinaweza kuhatarisha amani ya nchi kama ilivyotokea
katika nchini ya Rwanda na kupelekea mauaji ya kimbari nchini humo.
|
No comments:
Post a Comment