Kampuni ya
Facebook inayomiliki huduma ya Whatsapp imesema kuna baaadhi ya simu za zamani
zikiwemo zile zinazotumia mfumo wa Windows Phone 7.1, Android 2.2 na simu aina
ya iPhone 3GS/iOS hazitakuwa na huduma za whatsapp kwa sababu wanataka kuendana
na mifumo inayotumiwa na watu wengi.
Hatua hiyo
ilitangazwa na Facebook mapema ya mwezi february mwaka 2016 ambapo huduma ya
whatsapp ilitakiwa kuacha kazi katika mifumo hiyo ya programu mwishoni mwa
Desemba 2016 na ilikuwa imeorodhesha
simu za BlackBerry OS, BlackBerry 10, Nokia S40 na Nokia Symbian S60 kuwa
miongoni mwa simu ambazo zingekatiwa huduma mwishoni mwa mwaka 2016 lakini
ikabadilisha uamuzi wake na kuongeza muda hadi Juni 30, 2017.
Kampuni hiyo
imesema wakati wa kuanzishwa kwa WhatsApp mwaka 2009, asilimia 70 ya simu
wakati huo zilikuwa za BlackBerry na Nokia hivyo imeshauri wanaotumia simu za
aina hiyo kununua simu za kisasa zaidi.
|
No comments:
Post a Comment