Kombe la Mapinduzi 2017 - Yanga SC yachungulia Nusu Fainali kutoka Kundi B. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, January 04, 2017

Kombe la Mapinduzi 2017 - Yanga SC yachungulia Nusu Fainali kutoka Kundi B.

Mashindano ya Kuwania Kombe la Mapinduzi 2017 ambayo ni Mashindano ya kuenzi Miaka 53 ya Mapinduzi tukufu ya Visiwa vya Zanzibar na Pemba, yameendelea Leo,January 04,2017 kwa Timu ya Yanga SC kupata ushindi wake wa pili wa Kundi B.

Yanga SC ambao walianza kwa kishindo Kundi B kwa kuinyuka Jamhuri ya Pemba 6-0, wameichapa Zimamoto ya Zanzibar 2-0 kwa Bao za Dakika za 11 na 21 za Simon Msuva.

Yanga SC waliotawala Mechi hii, wangeweza kupata Bao la 3 walipopewa Penati kwenye Dakika ya 50 lakini Penati hiyo iliyopigwa na Simon Msuva ilichezwa na Kipa wa Zimamoto.
Matokeo haya yamewaweka Yanga SC kwenye nafasi nzuri mno ya kutinga Nusu Fainali ingawa kwa hali ilivyo unaweza tu kutamka tayari wapo Nusu Fainali.

Hadi sasa Msuva ndiye anaongoza katika orodha ya wafungaji akiwa na magoli manne akifatiwa kwa karibu na Labama mwenye magoli matatu.

January 07,2017, Yanga SC Kukamilisha Mechi zao za Kundi B kwa kucheza  na Azam FC mchezo wa tatu katika hatua ya makundi mechi inayosubiriwa kwa hamu na wapenzi wote wa soka kutokana na upinzani uliopo kati ya vilabu hivi viwili.
MSIMAMO.

KUNDI A.


NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
SIMBA
2
2
0
0
3
1
2
6
2
URA
2
1
0
1
3
2
1
3
3
JANG’OMBE BOYS
2
1
0
1
2
2
0
3
4
TAIFA JANG’OMBE
2
1
0
1
2
2
0
3
5
KVZ
2
0
0
2
0
3
-3
0





KUNDI B.



NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
YANGA
2
2
0
0
8
0
8
6
2
AZAM
1
1
0
0
1
0
1
3
3
ZIMAMOTO
2
0
0
2
0
3
-3
0
4
JAMHURI
1
0
0
1
0
6
-6
0

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad