Arsenal
imeambulia sare ya kufungana bao 3-3 na kupata alama moja nyumbani kwa
Bournemouth baada ya kutoka nyuma kwa magoli 3-0.
Alexis
Sanches alianza kuiandikia bao la kwanza Arsenal dakika ya 70 kabla ya Lucas
Perez kuandika bao la pili dakika tano baadae.
Bournemouth
ilianza kuyumba baada ya nahodha wake Simon Francis kulimwa kadi nyekundu
dakika ya 83 na kuachia mwaya kwa Arsenal kuutawala zaidi mchezo ambapo dakika
ya 90, Olivier Giroud aliisawazishia timu yake na kupelekea kugawana alama moja
moja.
Kwa matokeo
hayo Arsenal wanasalia katika nafasi ya nne wakiwa na alama 42 huku AFC
Bournemouth wakipanda mpaka nafasi ya tisa wakiwa na alama 25 kibindoni.
|
No comments:
Post a Comment