Ligi Kuu England 2016/2017: Manchester United Waitandika West Ham United Bao 2-0. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, January 03, 2017

Ligi Kuu England 2016/2017: Manchester United Waitandika West Ham United Bao 2-0.

Manchester United wamepata ushindi wao wa 6 mfululizo kwenye  Ligi Kuu England 2016/2017, kwa kuitandika West Ham United Uwanjani kwao London Stadium Jijini London Bao 2-0.

Dakika ya 13 West Ham walipata pigo kwa Mchezaji wao kutoka Algeria, Sofiane Feghouli kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu kwa Rafu mbaya aliyomchezea Sentahafu wa Man United ,Phil Jones.
Dakika ya 63, kazi njema ya Rashford kwenye Winga ya Kushoto ilimpa nafasi ya kumpasia Juan Mata na kuipa Man United Bao la kwanza.

Dakika ya 78 pasi ya Ander Herrera ilimkuta Zlatan Ibrahimovic aliandika Bao la Pili kwa Man United.

Kwa West Ham hiki ni kipigo chao cha 4 London Stadium Uwanja mpya walioanza kuucheza Msimu huu baada ya kuhama Upton Park na wapo Nafasi ya 13 huku Man United wakibakia Nafasi ya 6 lakini wako Pointi sawa na Tottenham iliyo Nafasi ya 5.

MATOKEO YA MECHI ZINGINE.

Jumatatu Januari 02,2017.

Middlesbrough 0 – 0 Leicester City 
           
Everton 3 – 0 Southampton    
        
Manchester City 2 – 1 Burnley   
               
Sunderland 2  - 2 Liverpool    
         
West Bromwich Albion 3  - 1 Hull City  
              
EPL – Ligi Kuu England

Jumanne Januari 03,2017.

2245 Bournemouth v Arsenal    
           
2300 Crystal Palace v Swansea City    
           
2300 Stoke City v Watford       
  
Jumatano Januari 04,2017.

2300 Tottenham Hotspur v Chelsea          

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad