Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Jana Jumatatu Januari 02, 2017 amemaliza ziara yake ya
siku mbili Mkoani Kagera kwa kuwatembelea baadhi ya wananchi walioathiriwa na
tetemeko la ardhi pamoja na kukagua baadhi ya miundo mbinu iliyoathiriwa na
tetemeko hilo na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa majengo ya shule ya sekondari
ya Ihungo Omumwani iliyobomolewa na
tetemeko la ardhi la Septemba 10,2016.
Mara baada
ya ukaguzi huo Rais Dkt Magufuli akazungumza na wananchi wa Mkoa huo wa Kagera
katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Ihungo na kuagiza kuvunjwa kwa kamati
ya maafa ya Mkoa huo iliyokuwa ikiratibu utoaji wa misaaada na kufanya tathmini
ya athari ya tetemeko hilo.
”Kila kitu
huwa kina mwanzo na mwisho wake ukiwa na harusi huwa kuna kamati ya
harusi,ukishamaliza kufunga ndoa kamati ya harusi huwa inavunjwa,na ukiwa
kwenye msiba huwa kuna kamati ya msiba na msiba
mkishazika kamati ya mazishi huvunjwa,kamati ya maafa ya Kagera huu ni
mwezi wa tano na inawezekana hata kwenye kamati huwa wanalipana posho,sasa
nataka hii kamati nayo iishe,yalishapita yamepita”
Aidha Dkt
Magufuli amewataka wote walioahidi kuchangia katika kamati ya tetemeko la ardhi
ya mkoa wa Kagera ambao bado hawajatekeleza ahadi zao ambazo ni jumla ya
shilingi bilioni nne nukta tano wakamilishe ahadi hizo ili ziweze kumalizia
miundombinu ya Serikali iliyoathiriwa na tetemeko hilo.
Ameongeza
kuwa wale wote wanaoendelea kuguswa kusaidia wapeleke michango yao moja kwa
moja kwa wananchi badala ya kuipeleka serikalini kwa kuwa hakuna mchango
mwingine utakaopokelewa katika Ofisi ya Waziri Mkuu.
Pia Rais Dkt
Magufuli ameagiza shule ya Sekondari ya Omumwani iliyokuwa inamilikiwa na
Jumuia ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi CCM imilikiwe na Serikali kutaka
wanafunzi wote wanaosoma katika shule hiyo kutolipa ada kama zilivyo shule
nyingine za serikali.
Dkt Magufuli
ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Kagera kupunguza utitiri wa kodi katika zao la
kahawa ili bei ya zao hilo ipande na kuwanufaisha wakulima
Balozi wa
Uingereza hapa Nchini Bi Sarah Cooke ambaye nchi yake imechangia kiasi cha
shilingi bilioni sita kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Sekondari ya Ihungo,
amempongeza Rais Dkt Magufuli na serikali yake kwa jitihada za kupambana na
rushwa suala ambalo nchi yake ya Uingereza inalipa kipaumbele sambamba na kutoa
elimu bila malipo jambo linalowawezesha watoto wengi wa kitanzania kupata elimu
bure
Jaffar Haniu
Naibu
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Kagera.
02 Januari,
2017.
|
No comments:
Post a Comment