Mapinduzi Cup 2017:Yanga SC Yaifumua Jamhuri ya Pemba Bao 6-0. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, January 02, 2017

Mapinduzi Cup 2017:Yanga SC Yaifumua Jamhuri ya Pemba Bao 6-0.

Timu ya Yanga SC wameanza Mechi zao za Kundi B la Kombe la Mapinduzi 2017 ambayo ni Mashindano ya kuenzi Miaka 53 tangu Mapinduzi tukufu ya Visiwa vya Zanzibar na Pemba, kwa kishindo kikubwa kwa kuifumua Jamhuri ya Pemba Bao 6-0.

Hadi Mapumziko Yanga SC ilikuwa ikiongoza kwa bao 4 – 0 dhidi ya Jamhuri , kwa Bao za Simon Msuva, Dakika za 19 na 40, na Donald Ngoma, Dakika za 23 na 37.

Kipindi cha Pili Yanga SC walipiga Bao nyingine 2 kupitia Thaban Kamusuko na Juma Mahadhi.

Mechi inayofuata kwa Yanga SC kwenye Mapinduzi Cup 2017 ni Jumatano dhidi ya Zimamoto ambayo mapema Leo,January 02,2017  ilifungwa 1-0 na Azam FC.
Azam FC imepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Zimamoto katika mchezo wa Kundi B michuano ya Mazpinduzi Cup inayoendelea visiwani Zanzibar.

Goli pekee katika mchezo huo limefungwa na Shabani Idd dakika ya 76 kipindi cha pili baada ya kufanikiwa kumpita golikipa wa Zimamoto kisha kufunga bao hili kiulani.


Jumanne Januari 3,2017 zipo Mechi 2 za Kundi A wakati Jang'ombe Boys wakicheza na Mabingwa Watetezi URA kuanzia Saa 10 Jioni na KVZ kuivaa Simba SC Saa 2 na Nusu Usiku.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad