Halmashauri ya Ngara mkoani Kagera kutoa Vitambulisho kwa Wazee 14, 270 0 ili kupatiwa huduma ya Afya bure. - Mwana Wa Makonda
cV7ufzj

Muhtasari

X-BET

MAIN-

Post Top Ad

cV7ufzj

Monday, December 19, 2016

demo-image

Halmashauri ya Ngara mkoani Kagera kutoa Vitambulisho kwa Wazee 14, 270 0 ili kupatiwa huduma ya Afya bure.

.com/simgad/
15542318_1295196343887090_8044874186358479527_n
Pichani,Kaimu Katibu mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka akiwapatia vitambulisho  baadhi ya Wazee wa kijiji cha Mumiramira kata Bugarama wilayani Ngara mkoani Kagera ambao Wana zaidi ya miaka 60 ili waweze kupatiwa huduma ya matibabu bure kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.
15492330_1295196273887097_882442590032687727_n
Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera inatarajia kutoa vitambulisho kwa wazee 14, 270 wenye umri zaidi ya miaka 60 ili waweze kupatiwa huduma ya matibabu bure kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kuanzia Januari, 2017.

Mwenyekiti wa Halmsahauri ya wilaya ya Ngara Bw Erick Nkilamachumu ametoa taarifa hiyo leo –December 19,2016 kwa Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM ngazi ya Taifa Bw Shaka Hamdu Shaka baada ya kutembelea wazee walioko kata ya Bugarama wilayani Ngara akiwa kwenye ziara ya utekelzaji ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020.

15541110_1295196353887089_6962769328893099675_n
 
15590516_1295196287220429_6986442153756237977_n
Bw Nkilamachumu amesema kwa awamu ya kwanza wazee wa kata ya Bugarama wapatao 390 wamepata vitambulisho hivyo na kwamba mkakati wa halmashauri ni kutoa huduma kwa wazee wote wenye zaidi ya miaka 60 hata kama hawajapatiwa vitambulisho ili mradi hajiwezi kiuchumi.

Hata Hivyo Kaimu katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM ngazi ya Taifa Shaka Hamdu Shaka ameitaka jamii kuwaenzi na kuwatunza wazee ili wazidi kuishi na kwamba wazee hao ni hazina kwa kuwa maendeleo yanayopatikana yanatokana na misingi yao ya uzalendo wa nchi yao.

15542318_1295196343887090_8044874186358479527_n

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Contact Form

Name

Email *

Message *