Donald J. Trump Ni mtoto wa nne wa mmiliki raslimali za majengo jijini
New York, Fred Trump.
Licha ya utajiri
wa familia yake, alitumainiwa kufanya kazi za daraja la chini zaidi katika
kampuni ya baba yake ambapo alipelekwa kujiunga na jeshi akiwa na umri wa miaka
13.
Baada ya hapo alijiunga na Chuo Kikuu cha Pennysylvania na akajiweka
katika nafasi nzuri ya kurithi utajiri wa baba yake baada ya kaka yake mkubwa,
Fred, kuwa rubani.
Fred Trump alifariki akiwa na umri wa miaka 43 kutokana na ulevi na
uvutaji sigara.
Ufanisi wake katika utajiri wa familia yake umemwezesha kuwa tajiri
mkubwa anayemiliki miradi mbalimbali mikubwa ikiwa ni pamoja na majumba,
mahoteli, na miradi mbalimbali iliyotapakaa Marekani, Mumbai, Istanbul na
Ufilipino.
Utajiri huohuo umemfanya tangu mwaka 1996 hadi 2015 kuyamiliki mashindano ya urembo ya Miss
Universe, Miss USA, na Miss Teen USA.
Pia amewahi kuandika vitabu kadhaa na ana biashara ya kuuza tai na maji
ya kwenye chupa kwa kiwango cha kimataifa na gazeti la Forbes limeuweka utajiri
wake katika kiwango cha Dola za Marekani bilioni 3.7 japokuwa yeye kila mara
amesema utajiri wake ni Dola za Marekani bilioni 10.
|
No comments:
Post a Comment