VINARA
wa Ligi Kuu Vodacom, Simba SC Leo Novemba
09,2016 wameshushiwa kipigo chao cha pili mfululizo baada ya kuchapwa 2-1 na
Tanzania Prisons huko Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Jumapili
iliyopita, Simba SC , wakiwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, walifungwa 1-0 na
African Lyon.
Leo, Simba
SC walitangulia kufunga Dakika ya 43 kwa Bao la Jamal Mnyate na Prisons
kusawazisha Dakika ya 47 kupitia Victor Hangaya ambae ndie pia alifunga Bao la
Pili na laushindi kwa Prisons katika Dakika ya 63.
Matokeo haya
yamewapaisha Tanzania Prisons hadi Nafasi ya 7 wakiwa na Pointi 19 kwa Mechi
15.
Simba SC
wanabaki kileleni wakiwa na Pointi 35 kwa Mechi 15 lakini pengo lao na Timu ya
Pili Yanga SC linaweza kupungua sana na kuwa Pointi 2 tu toka 8 za Wiki iliyopita
ikiwa Yanga SC Kesho Alhamisi wataibwaga Ruvu Shooting Uwanja wa Uhuru Jijini Dar
es Salaam.
|
No comments:
Post a Comment