Waziri wa
Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amezishauri kampuni
zinazotengeneza vilevi kutengeneza pombe yenye ladha ya gongo, kwa kuwa baadhi ya wateja wanavutiwa na ladha hiyo
wana wanakipenda kinywaji hicho.
Mwijage
ameyasema hayo leo bungeni mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa
Viti Maalumu, Gimbi Masaba (Chadema) aliyehoji mpango wa serikali wa kuanzisha
na kuhalalisha viwanda vya kutengeneza pombe aina ya gongo ili kuchochea uchumi
wa nchi na kubainisha kuwa, gongo ikitengenezwa kiwandani itafuata ubora
unaotakiwa kisheria.
“Moja ya
kigezo muhimu cha kuanzisha kiwanda ni uwepo wa soko, kutokana na wananchi
kupenda kinywaji hiki(gongo) nawashauri wadau wa sekta hii kuwasiliana na ofisi
za Sido ambazo zinapatikana mikoa yote ili kupata muongozo juu ya uanzishaji wa
viwanda bora na salama vya aina hii,” alisema Mwijage.
Amesema
haiwezekani Serikali kuhalalisha gongo, ila inaishauri sekta binafsi kuanzisha
viwanda vitakavyotumia malighafi zinazotengeneza kinywaji hicho kwa lengo la
kuzalisha kinywaji kinachokidhi viwango vya usalama na ubora wa chakula.
Katika swali
la nyongeza, Masaba amehoji kama serikali ipo tayari kufanya utafiti kujua
faida zilizo kwenye gongo.
Mwijage
amesema faida zinafahamika, lakini atawaelekeza wataalamu wake waendele maeneo
yenye gongo na pombe nyingine za kienyeji ili kuzifanyia utafiti na
zitengenezwe kwa kufuata ubora na viwango.
|
No comments:
Post a Comment