Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na
Ufundi iweke mpango maalumu wa kuongeza wataalamu zaidi katika sekta ya
afya ndani ya nchi ili kuipunguzia Serikali gharama za kusomesha
wataalam hao nje ya nchi.
Waziri
Majaliwa Ametoa agizo hilo wakati alipokua akikagua maendeleo ya mradi
wa ujenzi wa Kampasi ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya na Sayansi ya Tiba
Muhimbili (MUHAS) na Ujenzi wa Kituo cha Tiba cha Kimataifa cha
Muhimbili katika eneo la Mloganzila.
Amesema
Serikali zilizotangulia zimefanya kazi kubwa na nchi imefikia hatua
nzuri ya kuongeza wataalam ndani ya nchi ambao watakwenda kutatua
changamoto ya upungufu wa madaktari bingwa kwenye hospitali za mikoa na
wilaya.
Waziri
Mkuu amesema ujenzi wa kituo hicho cha tiba cha kimataifa pia
utawapunguzia wananchi adha ya kutafuta fedha za kwenda kupata matibabu
nje ya nchi.
Aidha
Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Bwana. Humphrey
Polepole awatafute watu wote waliohusika na wizi wa lita 1,000 za mafuta
ya kuendeshea mitambo katika karakana ya mkandarasi anayejenga Kampasi
hiyo ya MUHAS
“Wafanyakazi
waache wizi. Lita 1,000 zinaondokaje katika karakana ya mkandarasi? Hii
kampuni inayolinda kama imeshindwa kazi iondolewe na Mkuu wa wilaya
usimhurumie mwizi,” amesema Waziri Majaliwa.
Lakini
pia Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako
amesema kukamilika kwa kampasi ya Mloganzila kutasaidia upatikanaji wa
madaktari bingwa wengi nchini ambao watapunguza gharama za kupeleka
wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi.
Awali,
Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa. Ephata Kaaya alisema kukamilika kwa
hospitali pamoja na kampasi ya chuo kutawezesha kupunguza kwa kiasi
kikubwa uhaba wa wataalamu wa afya nchini.
Pamoja na msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Ujenzi
wa mradi huo umegharimu Dola za Kimarekani milioni 61, ambapo Serikali
imetoa Dola milioni 18 na Serikali ya Korea imetoa mkopo wa Dola milioni
43. Kukamilika kwa ujenzi wa kampasi hiyo ya Mloganzila
kutawezesha chuo kuongeza idadi ya udahili wa wanafunzi wa fani ya afya
kutoka 4,010 hadi 15,000.
Prof. Kaaya
amesema mkataba wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa mradi huo ulisainiwa
tarehe 12, Desemba, 2014 na ujenzi ulianza mwezi Julai, 2015 na
unatarajiwa kukamilika Oktoba, 2016.
Na Hashim Ibrahim (UDSM-SJMC)
Baadhi ya wafanyakazi na Wananchi wa eneo la Mloganzila
Waziri Mkuu akionyeshwa moja ya mashine zilizopo hapo
moja ya mashine zilizopo hapo
Baadhi ya wafanyakazi wakifuatilia tukio hilo
No comments:
Post a Comment