Taifa Stars yashindwa kuifunga Nigeria na yakubali kipigo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, September 03, 2016

Taifa Stars yashindwa kuifunga Nigeria na yakubali kipigo.

Timu ya Taifa ya Tanzania-Taifa Stars imehitimisha mechi za Kundi G kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kufungwa bao 1-0 na wenyeji, Nigeria jioni ya leo Uwanja wa Uyo, Akwa Ibom.

Bao pekee la Super Eagles limefungwa na mshambuliaji wa Manchester City, Kelechi Iheanacho dakika ya 78 katika mchezo uliokuwa mkali na wa kusisimua.  

Mchezo wa kwanza wa Taifa Stars dhidi ya Nigeria ulichezwa September 05 2015 uwanja wa Taifa Dar es Salaam na ulimalizika kwa suluhu ya 0-0, hiki ni kipigo cha 5 Taifa Stars kufungwa na Nigeria katika mechi zake nane walizowahi kukutana, Taifa Stars haijawahi kuifunga Nigeria na wameambulia sare 3 kati ya mara 8 walizokutana.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad