Wakala wa Jiolojia Nchini Aelezea ukubwa wa Tetemeko Lililotokea Septemba 10,2016 Katika Mikoa Ya Kanda ya Ziwa likiua zaidi ya Watu 10 na Kujeruhi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, September 11, 2016

Wakala wa Jiolojia Nchini Aelezea ukubwa wa Tetemeko Lililotokea Septemba 10,2016 Katika Mikoa Ya Kanda ya Ziwa likiua zaidi ya Watu 10 na Kujeruhi.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Profesa Abdulkarim Mruma amesema Tetemeko  la ukubwa wa mtikisiko wa kipimo cha Ritcher 5.7 limetokea katika mikoa mitatu nchini na watu zaidi ya 10 wamekufa na wengine 120 wamejeruhiwa huku majengo mengi yakibomoka, ni kubwa kwa nusu ya kipimo cha juu cha Ritcher 10 na limezidi kipimo cha chini cha ukubwa wa Ritcher tatu.

Profesa Mruma amesema tetemeko hilo limetokea katika mpaka wa Tanzania na Uganda, kilometa 47 kaskazini mwa Bukoba mkoani Kagera na sababu ni mpasuko wa ardhi katika Bonde la Ufa la magharibi karibu kabisa na Ziwa Victoria .
Mikoa iliyoripotiwa kuathiriwa kwa tetemeko hilo ni Kagera, Mwanza na Mara. Pia tetemeko hilo limeukumba mji wa Kampala na Rakai nchini Uganda jana Septemba 10,2016.

Amewataka wananchi kuchukua tahadhali kwani kwa kawaida linapotokea tetemeko kubwa kama hilo hufuatiwa na matetemeko madogo na ardhi hutulia baada ya siku mbili mpaka tatu.

Kwa wakati huu ili kuepuka madhara zaidi, litakapotokea watoke nje ya nyumba na kukaa mbali na miti kwenye uwanja wa wazi na wanaoendesha magari waache mara moja,” amesema Profesa Mruma.
Amesema kwa sasa wataalamu katika kituo chao cha kupimia matetemeko cha Geita wanaendelea kupata takwimu zaidi kutokana na kuwa mpasuko wa tetemeko hilo umekuwa karibu sana na ziwa Victoria na baadaye watatoa taarifa kuhusu tukio hilo kwa undani.
Sababu ya Vifo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi amesema tetemeko hilo limetokea saa tisa alasiri na zaidi ya watu 10 wamekufa.

Amesema tisa kati ya waliokufa ni wakazi wa Manispaa ya Bukoba na mmoja ni mkazi wa wilayani Karagwe.

Kamanda amesema miongoni mwa majeruhi wamo wanafunzi 15 wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihungo na wapo katika hospitali ya mkoa wanaendelea kupatiwa huduma. Alisema bado vikosi vya uokoaji likiwemo Jeshi la Polisi na Zimamoto vinaendelea na uokoaji.

Amesema watu waliojeruhiwa na waliokufa wamedondokewa na kuta, vifusi na vyombo vya ndani.
Amesema wengine walikufa kwa mshituko unaosababishwa na shinikizo la damu na nyumba zaidi ya 40 zimeathirika.

Ni kweli tetemeko la ardhi limetokea na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali za watu, vifo pamoja na majeruhi na bado tunaendelea kupokea taarifa zaidi,” alisema Kamanda Ollomi na kuongeza kuwa mpaka jana Septemba 10,2016, jioni walikuwa wakiendelea kupokea taarifa kutoka sehemu mbalimbali za mkoa huo kuhusu vifo na majeruhi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad