Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2016/2017 - Simba SC 2 - 0 Mtibwa Sugar F.C. | Ajibu 52’ Mavugo 56’ - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, September 11, 2016

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2016/2017 - Simba SC 2 - 0 Mtibwa Sugar F.C. | Ajibu 52’ Mavugo 56’

Timu ya soka ya Simba SC imerudi kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu 2016/2017 baada ya kuifikia kwa pointi Azam FC kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar jioni ya leo,Septemba 11,2016 katika mchezo ulipochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Shukrani kwao, wafungaji wa mabao hao, Ibrahim Hajib na Laudit Mavugo yote kipindi cha pili na sasa Simba SC inafikisha pointi 10 baada ya kucheza mechi nne, wakishinda tatu na sare moja.
Hajib alifunga dakika ya 52 kwa kichwa akimalizia kona nzuri iliyochongwa na beki Mohammed Hussein 'Tshabalala', wakati Mavugo alifunga dakika ya 66 akiwa ndani ya boksi baada ya pasi ya kiungo Mwinyi Kazimoto.

MATOKEO MENGINE YA LIGI KUU VODACOM TANZANIA BARA 2016/2017.

Jumamosi Septemba 10,2016.

Mwadui FC 2 – 2 Stand United

Mbeya City 1 – 2 Azam FC

Ndanda FC 0 – 0 Kagera Sugar

Yanga 3 – 0 Majimaji FC

Ruvu Shooting 1 – 0 JKT Ruvu

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad