Wafahamu Wachezaji 20 wa Taifa Stars wa Kuivaa Nigeria September 03. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, August 25, 2016

Wafahamu Wachezaji 20 wa Taifa Stars wa Kuivaa Nigeria September 03.

Uwanja wa Uwanja wa Uhuru.

Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa, ametangaza wachezaji 20 watakaounda kikosi kitakachosafiri mwishoni mwa mwezi huu kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017) dhidi ya timu ya taifa ya nchi hiyo, Super Eagles.

Licha ya mchezo huo wa Septemba 3, 2016 kuwa sehemu ya mchuano wa kuwania nafasi ya kucheza fainali hizo za AFCON 2017 huko Gabon, lakini utakuwa ni wa kukamilisha ratiba baada ya Misri kufuzu kutoka kundi G ambalo mbali ya Nigeria na Tanzania, pia ilikuwako Chad ambayo iliyojitoa katikati ya mashindano.

Tanzania hatuwezi kupuumza mchezo huu, tumeuchukulia serious (kwa umakini) kabisa kwa sababu tunacheza ugenini ambako matokeo mazuri yanaweza kutusongesha mbele na kuingia ndani ya timu 99 bora katika viwango vya FIFA,” amesema Mkwasa.

Katika kikosi chake, Mkwasa ametangaza kutomjumuisha Mshambuliaji wa Kimataifa, Thomas Ulimwengu anayecheza klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kutokana na majeruhi ya paja kama ilivyo kwa Juma Abdul wa Young Africans ambaye aliumia katika mchezo wa kuwania Kombe la Shirikisho dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria.

Timu itaingia kambini Agosti 28, itakaa kambini kwa siku tano kabla ya kusafiri kucheza mchezo huo wa kukamilisha ratiba ambao Misri tayari wameshafuzu fainali za Afrika,” amesema Mkwasa na kuongeza kuwa kuna mchezaji wa Tanzania, Said Carte Mhando anamfuatilia ili ikiwezekana baadaye amwite kuchezea timu ya taifa. Anakipiga Klabu ya Brencia Calcio ya Italia.

Wachezaji walioitwa:

Makipa

Deogratius Munishi – Young Africans

Aishi Manula – Azam FC

Mabeki

Kelvin Yondani - Young Africans

Vicent Andrew - Young Africans

Mwinyi Haji - Young Africans

Mohamed Hussein – Simba SC

Shomari Kapombe - Azam FC

David Mwantika - Azam FC

Viungo

Himid Mao - Azam FC

Shiza Kichuya – Simba SC

Ibrahim Jeba – Mtibwa Sugar

Jonas Mkude – Simba SC

Muzamiru Yassin – Simba SC

Juma Mahadhi - Young Africans

Farid Mussa Tenerif ya Hispania

Washambuliaji

Simon Msuva - Young Africans

Jamal Mnyate – Simba SC

Ibrahim Ajib – Simba SC

John Bocco - Azam FC

Mbwana Samatta - CK Genk ya Ubelgiji

IMETOLEWA NA TFF

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad